Burudani

Ukiongelea video za muziki Tanzania huwezi kuacha kuwataja waongozaji hawa watano!

Maisha yanaenda kasi mno. Leo muziki wa Bongo Flava umebadilika kwa kiasi kikubwa tofauti na miaka kadhaa nyuma. Leo mashabiki wamekuwa wakihitaji video nzuri na sio kusikiliza wimbo mzuri peke yake. Mashabiki wanaamini wimbo mzuri unabebwa na video nzuri.

micromb_red_lg

Hawako mbali na ukweli kwakuwa leo tunamuona Diamond kama msanii mkali zaidi kwenye Bongo Flava anayetamba Afrika nzima lakini siri ya mafanikio yake ni kukubali kuingia gharama na kufanya video kali zenye kueleweka hata na media za nje ya nchi.

Tumemuona Alikiba ambaye video zake za awali zote zilikuwa za kawaida lakini kwa ‘kelele’ za mashabiki aliamua kufunga safari mpaka Cape Town,South Africa kwa Godfather kwenda kufanya video ya Mwana.

AY amekuwa akifunga safari ndefu mpaka Marekani kwenda kufanya video za nyimbo zake huku wengine wakikimbilia Kenya yote ni kutaka kitu bora ni rahisi zaidi kumshawishi na kumteka shabiki asiyejua kiswahili kwa video kali kuliko kwa audio kali.

Orodha hii inakuletea waongozaji watano wa video nchini waliotawala zaidi soko la ufanyaji video za Bongo Flava.

Adam Juma

https://www.youtube.com/watch?v=nw59lY5hpF4

Unaweza kumwita Godfather wa hii kitu. Alikuwepo toka mwanzo kabisa wakati ambao hakukuwa na mabadiliko kama ilivyo leo. Alitengeneza video ya ‘Mbagala’ ya Diamond ambayo ilimfanya Diamond achaguliwe kuwania tuzo za MTV MAMA mwaka 2010.

Video ya Witness ‘Zero’ pia ilipata kugombea tuzo za Channel O bila kuwasahau Shaa na Cpwaa ambao video zao zenye mikono ya Adam Juma zilipata bahati ya kutajwa kwenye tuzo nyingi kubwa za Afrika.
Mwaka 2013 kwa kushtukiza na bila kutegemewa alitangaza ujiweka pembeni ya game na kufanya vitu vingine.

Mwaka jana alirudi tena kwenye game na bila shaka alirudi akiwa na nguvu mpya, jina jipya ‘AJ’ na idea mpya na ambazo zimekuja kuleta mabadiliko.

‘Pacha Wangu’ Rich Mavoko, Forever ya Jide,Tupogo ya Ommy Dimpoz na Nitakupwelepweta ya Yamoto Band, Vuvula ya raisi wa Manzese, Madee na wimbo mpya wa Christian Bella Nashindwa ni mifano michache ya kazi nzuri mpya za AJ.

Khalfan

Mara nyingi amekuwa sio muongeaji mzuri kwa kiasi hicho ameacha kazi zake ziongee zenyewe. Zamani alikuwa ni kijana wa Nisher ila walikuja kupishana kauli na Khalifan kuamua kujitoa kwa Nisher na kwenda kuanzisha kampuni yake ya video. ‘I Just Wanna Love’ ya Aika na Nahreal ilikuwa video yake iliyofungua vitu vingi kwenye maisha yake.

Vitamin Music ya Belle 9 na Joh Makini ni video kali mno yenye maudhui tofauti ambayo imempeleka mbele Khalfani kutoka kule alipokuwa. Na huwezi kushangaa ukiona kuwa hata wimbo wa Quick Racka ‘Bishoo’ ulifanywa na kijana huyu.

Hivi karibuni Khalfan ameongoza video ya wimbo wa Ben Pol, Sophia ambayo imekuwa kuwa oja kati ya vitu vikubwa kutoka kwake.

Hanscana

The Big Name in Town. Utasema nini zaidi juu ya ‘Arusha Boy’ huyu ambaye ameamua kuweka makazi yake Dar na kufanya video nzuri!

Ni muongeaji mzuri mno kushinda mshkaji wake Khalifan na sio mdomo wake tu unaofanya kazi hata kichwa chake maridadi kimekuwa kikitoa video kali ambazo zimeshindwa kutegemewa kama zingeweza kutoka kwake.
Video kama Siri ya Barnaba na Vanessa Mdee,Moyoni ya Aika na Nahreal zote zimepata nafasi VEVO.

Director anaYefanya vizuri Kenya kwa sasa Kevin Bosco ametoa ya moyoni kwa kusema Hanscana ni director anayemkubali zaidi bongo kwa wakati huu na hivi karibuni video ya Roma Mkatoliki ya wimbo wake ‘Mwanakondoo’ itaongeza idadi ya video alizoongoza.

Hata hivyo video ya ‘Nasema Nawe’ imekuwa ni kitu kikubwa kwake na kimempeleka kule alipotaka kwenda siku zote. Video hiyo hadi sasa ina zaidi ya views milioni 1.2 ikiwa haijamaliza hata mwezi tangu iwekwe Youtube.

Kitu kikubwa zaidi Hanscana atakuwa muongozaji wa video wa tatu Bongo kufanya kazi na Prince Diamond, ukimtoa Raqey aliyetengeneza ‘Nataka Kulewa’ na Adam Juma.

Bila shaka kazi hii na Diamond itafungua vitu vingi vikubwa kwake kama ilivyofungua kwa producer Sheddy Clever baada ya kutengeneza hit ya Number One!

Nisher

Jikubali ya Ben Pol ilichezwa mpaka Channel O na MTV. Yalikuwa ni mafanikio makubwa kwake. Huku wimbo wa Nje ya Box ya Weusi ikionyesha jinsi gani alivyo muongozaji huyu mkomavu. Game imebadilika mno na ushindani umekuwa mkubwa kiasi sasa Nisher hayupo pale alipotaka kuwa na mwenyewe amekiri hiyo kitu.

Wakati fulani alikuwa mshindani mkubwa zaidi wa Adam Juma ila leo imekuwa tofauti ambapo wamekuja vijana wengi wanaofanya vizuri kwenye game ila video zake mbili za hivi karibuni kama 13 ya Young Killer na Bongo Hip Hop ya Fid Q zimezidi kumsimamisha vizuri pale alipo.

Nick Dizzo

Huyu ni mmoja kati ya mashujaa wasioimbwa. Video kama Love Me ya Mbeya boy, Izzo Bizness haikuishia kuchezwa na vituo vya ndani peke yake ilipata nafasi ya kutosha kwenye vituo vingi vya nje.
Amekuwa sio penzi mkubwa wa social network pengine ni moja kati ya vitu vinavyomfanya asiwe sana midomoni kwa watu ila ubora wa video zake ni kitu ambacho hakipaswi kuachwa hivi hivi. Amefanya vizuri pia kwenye video ya wimbo wa Izzo B ‘Kidawa’ aliomshirikisha Shaa.

Imeandikwa na Heri Best, unaweza kumfolow Instagram:Heri Best au Twitter:@MimiHeri

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents