Habari

Ukishiriki mwanafunzi wa kike au wakiume anayesoma shule kuolewa/kuoa adhabu kali inakuhusu

Serikali imesema ni marufuku kwa mtu yeyote kuoana na msichana au mvulana anaesoma shule ya msingi au sekondari na aatakaye shiriki adhabu kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Kauli hiyo na Naibu waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi, ajira na watu wenye ulemavu, Antony Mavunde akijibu kwa Niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Hawa Mwaifunga ambapo pia amesititiza kwa yeyote atakayeshiriki msichana au mvulana kuoa au kuolewa anakuwa ametenda kosa.

“Serikali inatambua umuhimu wa elimu kwa wototo wa kike na wa kiume wa Tanzania, hii inadhihirishwa na uamuzi wa serikali ya awamu ya tano wakuifanya elimu ya shule ya msingi na sekondari kuwa ya lazima na kutolewa bila malipo, lengo la mpango huu ni kuhakikisha watoto wetu wote hasa wa kike wanaipata elimu hii ya bila kikwazo,” amesema Mavunde leo Juni 22 Bungeni Jijini Dodoma.

“Kuzingatia elimu ya mtoto wa kike serikali imeendelea kuzingatia utekelezaji wa sera ya elimu ambayo inalinda haki za mtoto kusoma hadi sekondari kupitia marekebisho yaliyofanywa kwenye sera ya elimu na mabadiliko ya sheria mbalimbali namba mbili ya mwaka 2016 ni marufuku kwa mtu yoyote na katika mazingira yoyote kuoana na msichana au mvulana anaesoma shule ya msingi au sekondari pia ni kosa kumpa mimba mwanafunzi anayesoma shule ya msingi au sekondari na yeyote anaesaidia msichana au mvulana kuoa au kuolewa anakuwa ametenda kosa marekebisho haya yameweka adhabu kali kwa yoyote atakayetenda makosa haya,” amesisitiza.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents