Habari

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Firauni, Moyo wa binadamu wasahaulika kwenye Ndege

Ndege ya abiria ya Marekani iliyokuwa ikisafiri kutoka mji wa Seattle kuenda Dallas ililazimika kukatiza safari baada ya moyo wa binadamu kusahaulika ndani yake. Shirika la ndege la Southwest linasema kuwa kiungo hicho kilisafirishwa Seattle kutoka California, ambako ilitarajiwa kutolewa mishipa ambayo ingetumiwa baadaye kwa utaratibu wa tiba ya upandikizaji.

Lakini kisanduku ambacho kilikuwa kimehifadhi moyo huo kilisahaulika ndani ya ndege hiyo na hilo lilifahamika baada ya ndege kuanza safari kuelekea Dallas.

Kwa mujibu wa BBC, Kisa hicho kilitokea siku ya Jumapili lakini kiliangaziwa katika vyombo vya habari siku ya Alhamisi. Abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo wanasemakana kushutuka sana wakata rubani alipowaambia kuhusiana na mzigo huo na kwamba hana budi kugeuza mkondo na kurejea walikotoka.

Baadhi yao walitumia simu zao kujifahamisha kuhusu muda ambao moyo unaweza kuhifadhiwa kabla ya itumike kwa upasuaji- kwa mujiu wa wataalamu, moyo wa binadamu huchukuwa kati ya saa nne na sita kuharibika. Ndege hiyo iliripotiwa kupaa angani kwa karibu saa tatu.

Daktrai mmoja aliyekuwa miongoni mwa wasafiri na ambaye hakuwa na uhusiano wowote wa kusafirisha kiungo hicho aliiambia gazeti la Seattle Times, kwamba tukio hilo ni ”utepetevu wa hali ya juu”.

Baada ya ndege hiyo kutua salama mjini Seattle, moyo huo ulipelekwa katika kituo cha afya cha kuhifadhiwa. Gazeti hilo liliongeza kuwa kiungo hicho kilipokelewa na kuhifadhiwa katika muda uliyostahili.

by Ally Juma.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents