Burudani

Ukiwa WCB asilimia 90 ya ndoto zinatimia – Lukamba, Mpiga Picha wa Diamond (+video)

Mpiga picha wa Diamond Platnumz na WCB kwa ujumla, Lukamba amesema moja ya vitu ambavyo anajivunia kufanya kazi na muimbaji huyo ni kuweza kumkutanisha na watu mbali mbali.
Lukamba, Omario na Diamond

Lukamba amesema kuwa kuwepo ndani ya WCB kumemuwezesha kufikia baadhi ya ndoto zake za muda mrefu.

“Kuna wengine wanaweza kuwa wamezunguka lakini shughuli ninazofanya kwa Diamond nazunguka sana, nakutana na watu wengi na uzoefu mkubwa naupata,” Lukamba ameiambia Bongo5.

“Najiona mbali sana kwa sababu ukiwa WCB asilimia 90 ya ndoto zinakuwa zimetimia kwa sababu nilikuwa na dream ya kumuona Moe Musa, ni watu ambao nilikuwa nawasoma YouTube nimekuja nimekaa nao nime-share nao idea,” ameongeza.

Soma Pia; Mpiga picha wa Diamond ‘Kifesi’ aacha kazi WCB, atoa sababu mbili kubwa

Inaelezwa kuwa Lukamba ndiye amechukuwa nafasi ya Kifesi ambaye mwanzoni ndiye aliyekuwa official photographer wa Diamond Platnumz kabla ya kutangaza kuachana na kazi hiyo ndani ya WCB.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents