Diamond Platnumz

Ukubwa wa faida inayopatikana katika biashara ya miito ya simu wawanyong’onyeza wasanii

Faida inayopatikana kutokana na mauzo ya miito ya simu maarufu kama ring back tone, RBT, ni kubwa kiasi cha kuwafanya wasanii wa Tanzania wanyong’onyee kutokana na mgao kiduchu wanaopokea.

Black-woman-Smart-phone

Asilimia 75 ya faida ya biashara hiyo inayoingiza takriban shilingi bilioni 40 kwa mwaka huenda kwa makampuni ya simu, zaidi ya asilimia 30 huenda kwa makampuni ya kati yanayozungumza na wasanii ‘aggregators’ (mfano Push Mobile) na asilimia 2.5 huenda kwa wasanii.

Katika mjadala mrefu uliofanyika jana kupitia Twitter, mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alidai kuwa aliwahi kuoneshwa data za kampuni moja inayohusika na biashara hiyo ni kubaini kuwa Diamond pekee kwa mwezi mmoja aliingiza shilingi milioni 136 lakini alilipwa shilingi milioni 1.3 pekee.

Hata hivyo mbunge huyo ambaye kwa muda mrefu amekuwa akilipigia kelele suala hilo, amekanusha kutokuwa na maslahi katika biashara ya RBT.

“I repeat, I have no business interest.Mimi sio mfanyabiashara na sitafanya biashara hata ya nyanya nikiwa bado mwanasiasa,” alisisitiza Zitto.

“Wenye maslahi ya kibiashara kwenye #RBT wanadhani kila mtu ni kama wao. Mi Nataka artists wafaidi jasho lao basi. Tutaleta mabadiliko pia kwenye biashara ya #RBT hata wenye maslahi wapinge namna gani. Wadau wakubali dialogue kupata suluhisho.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents