Burudani

BIFU YA KIDUM NA HERMY B: UKWELI ULIOFICHIKA KUHUSU WIMBO WA NITAFANYA KIDUM FT LADY JAYDEE

Hivi karibuni kulitokea kutoelewana kati ya Producer Hermy B na masanii aliyekuja kwa kasi Kidum. Bongo5 iliamua kumtafuta Hermy B hili kuzungumzia nini chanzo cha Beef Yao. na Hermy hakusita kunitumia Email na kuelezea kila kitu.

Email kutoka B Hits…

Ngoja nitoe ukweli wa huu wimbo.

 

Kidum alipokuja Dar aliamua kumtafuta Hermy ambae alikutana nae project fame kule Nairobi. Wakakutana na kufanya kazi pamoja..katika maana ya kwamba mziki huu uliundwa na Hermy na Kidumu akitoa melodies. Drum Patern Yoote ni Ya hermy.

Kidum aliporudi kule Nairobi akakutana na Rkay(jamaa anaetengeneza mziki wa Wahu examples sweetlove, runin low) madhumuni ni kutengeneza video ya wimbo huu. Cha ajabu Rkay akamtengeneza kidum mpaka akakubali kurekodi upyaa wimbo huo. Rkay alikopi kila kitu ila akabadili sauti tofauti kidooogo, ila kisheria alibeba Idea ya kisanii ya Hermy kama ilivo. yote haya yalifanyika bila kuomba ruhusa wala kumpa taarifa Hermy.

Muda ulipofika Hermy alitoa huo mziki kwa radio stesheni, na kidumu alikimbilia kuomba wasiucheze huo wasubiri ule wa Rkay..alipoulizwa huu una tatizo lipi alishindwa kujieleza na akagundulika hana mantiki zaidi ya Ubaguzi wa sanaa tu. Stesheni flani flani wakakubali kuupokea na kuucheza huu wa kwetu Tanzania. Hermy hakutaka kuongea chochote kile mpaka alipoona wimbo huo wa Rkay ukichezwa na upo kwa video aliyopiga Rkay kwa sasa. Mwenye maskio na aliyeskia wimbo huu mara ya kwanza atajua tu huu uliopo kwenye video ni tofauti na vyombo vimepunguzwa, sio kwamba Rkay hajui kutengeneza muziki, ila alikua akijaribu kujitofautisha sana na Hermy na amejikuta akiharibu kiasi flani sanaa hiyo. Ninachoomba ni kwamba watanzania tuendelee kushikamana na kupeana suport kwenye wizi wa sanaa kama huu. Tuwe na cha kujivunia kwa watengeneza mziki wetu. Asalaamu!

 

PICHA ZA KIDUM NA HERMY USIKU WA KUREKODI WIMBO WA NITAFANYA

Hii ni video ya wimbo wa nitafanya

{youtube}WmuR1NUrvR0{/youtube}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents