Habari

Ulaya yachukizwa na mauaji ya Goerge Floyd, Ujerumani yaunga mkono maandamano Marekani

Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amesema kifo cha Goerge Floyd, Mmarekani mweusi aliyeuawa na polisi mweupe wiki iliyopita kilitokana na matumizi mabaya ya mamlaka, na kusema nchi 27 wanachama wa umoja huo zimeshtushwa na kuchukizwa na tukio hilo.

Trump was moved to bunker, sources confirm - ABC News

Borrell amesema vyombo vya usalama havipaswi kutumia uwezo wake kwa njia kama ile iliyosababisha kifo cha Floyd katika mazingira ya kusikitisha sana.

Wakati huo huo, waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani ameunga mkono maandamano ya amani yanayofanyika nchini Marekani kulaani ukatili wa polisi, akisema anayo matumaini kuwa yataleta mabadiliko.

Borrell pia amesema Umoja wa Ulaya unaunga mkono haki ya kufanya maandamano kwa amani, na unapinga aina zote za ghasia na ubaguzi. Hali kadhalika ametoa wito wa kupunguza mivutano nchini Marekani.

Baadhi ya polisi New York City wamenaswa na kamera wakiwa wanapiga picha na baadhi ya waandamanaji.Wakati huko katika jiji la Oklahoma City kamera pia zimenasa baadhi ya matukio ya polisi wakionekana kupiga magoti huku wengine wakiwakumbatia waandamanaji hao kama ishara ya kuonyesha umoja.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents