Tupo Nawe

Ulaya yalaani kitendo cha Uturuki kutumia wakimbizi kama kinga, kutekeleza operesheni zake Syria

Rais anayeondoka wa Baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk ameiambia Uturuki kutowatumia wakimbizi kama silaha ya kuulaghai Umoja wa Ulaya kuhusiana na suala la Syria.

Image result for Donald Tusk

Tusk amemkosoa vikali Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan kufuatia kitisho chake cha “kufungua milango” na kuwafukuza wakimbizi milioni 3.6 kama Umoja wa Ulaya utaiita operesheni yake nchini Syria kuwa ni “uvamizi”.

Akizungumza na waandishi habari mjini Nicosia, Cyprus, Rais huyo wa Baraza la Umoja wa Ulaya amesema Uturuki lazima ielewe kuwa hofu yao kubwa ni kuwa vitendo vyake huenda vikasababisha janga jingine la kibinaadamu.

Uturuki: Fahamu sababu za Rais Erdogan kutishia kuwaachia wakimbizi zaidi ya milioni 3 kuingia Ulaya

Mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ulishindwa kukubaliana taarifa ya pamoja kuhusu hatua hiyo ya Uturuki, huku wanachama wa Umoja wa Ulaya wakilaani hatua hiyo lakini nayo Urusi ikikataa kusaini taarifa hiyo.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW