Burudani ya Michezo Live

Ulaya yatoa orodha mataifa 14 kuanza safari, Marekani haipo

Mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana juu ya kile yanachokiita “orodha salama” kwa mataifa 14 ambayo yataruhusiwa kwa safari zisizo muhimu kuanzia Julai, huku Marekani ikiwa haimo kwenye orodha hiyo.

PHILIPPINES - EUROPEAN UNION The EU removes the ban: Philippine ...

Baraza la Umoja wa Ulaya limesema hapo jana kwamba nchi hizo salama ni Algeria, Australia, Canada, Georgia, Japan, Montenegro, Morocco, New Zealand, Rwanda, Serbia, Korea Kusini, Thailand, Tunisia na Uruguay.

Kundi hilo la mataifa 27 linatazamiwa kutoa muongozo unaolegeza au kuruhusu safari za matembezi ama kibiashara kuanzia kesho leo Jumatano kwa mataifa hayo.

Urusi na Brazil, kama ilivyo Marekani, hazikukidhi vigezo vya mataifa yaliyo salama kutokana na janga la COVID-19.

Uamuzi huu unakusudia kuunga mkono sekta ya usafiri na utalii barani Ulaya, hasa kwa mataifa ya kusini, ambayo yameathirika vibaya na janga la korona.

Related Articles

Back to top button
Close
Bongo5

FREE
VIEW