Michezo

Ulinzi mkali Urusi, United, Liverpool itakapo cheza klabu bingwa Ulaya

Kuelekea michezo ya Klabu Bingwa Barani ulaya mashabiki wa timu za Liverpool na Manchester United wameonywa kuwa wapole huko Moscow nchini Urusi kwa kuwa kutakuwa na maafisa wengi wa polisi katika mji huo.

Takriban mashabiki 2,000 watasafiri kuelekea kaskasini magharibi ambapo Liverpool itacheza dhidi ya Spartac Moscow siku ya Jumanne huku United ikikabiliana na CSKA Moscow siku ya Jumatano.

United imewaambia mashabiki wake kutovaa rangi za klabu hiyo ama hata kutembea Moscow wakiwa peke yao.

Liverpool inasema kuwa mamlaka ya Urusi inajua kwamba vilabu hivyo viwili viko mjini Moscow wakati mmoja kwa hivyo maafisa wengi wa polisi wanatarajiwa mahali popote ambapo mashabiki wa Liverpool na Manchester United watakongamana. Ikiwemo katika maeneo ya malazi.

Mashabiki sugu wa Urusi waliwashambulia wenzao wa Uingereza mjini Marseille katika kombe la bara la Ulaya mwaka 2016.

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents