Habari

Umaarufu wa YouTube wasababisha kifo (Video)

By  | 

Mwanamke mmoja kutoka nchini Marekani katika mjini wa Minesesotta amehukumiwa kwenda jela kwa kumuua mpezi wake.

Mwanamke aitwaye Monalisa Perez amehukumiwa kwa kumpiga risasi katika kifua mtu mmoja aitwaye Pedro Ruiz, ambaye ni mpenzi wake na wamezaa watoto wawili. Kitendo kilichofanya na mwanamke huyo kinaelezwa kuwa kilifanyika kwa masihara ilikuweza kutafuta umaarufu zaidi katika mtandao huo.

Watu takribani 30 walikuwa mubashara kuitazama video hiyo ilionesha mwanaume huyo akiwa amezuia risasi hiyo kwa kutumia kitabu hata hivyo ilipenye hadi katika kifua chake na kupelekea kufariki.

“Pedro alinieleza juu ya na mpenzi wake kufanya kitendo hicho kupitia YouTube iliwaweze kuwa maarufu, lakini nilimkataza na nikamuhoji kwa nini mtumie bunduki? hata hivyo wawili hao walipendana sana na walifanya mzaha huo kimakosa,” ameeleza Claudia Ruiz binamu wa marehemu kupitia kituo cha televisheni cha WDAY-TV.

Na Laila Sued

Jiunge na Bongo5.com sasa

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!

Add a comment

comments