Umaliziaji wako ndio utakaokupa heshima na sio jinsi ulivyoanza

Kuanza vizuri hakuna sifa kubwa kama kumaliza vizuri. Watu wengi huwa tunapenda kuanza kwa mbwembwe na matarumbeta mengi sana lakini tunashindwa kumalizia kila tunachokifanya vizuri. Ukifuatilia historia ya watu wengi ni kwamba walianza vizuri lakini wakashindwa kumalizia vizuri na watu wakawadharau kwa umaliziaji wao mbovu.

black-woman-thinking

Haijalishi umeanzaje bali utakavyomalizia itatupa picha wewe ni mtu wa namna gani. kama umeanza biashara na huduma nzuri halafu mwishoni hakuna huduma nzuri tunajua ya kuwa wewe ni kopo tupu zilikuwa ni kelele tu.

Utajiuliza hivi kwanini Mandela watu wanamheshimu sana? Ni namna alivyoweza kumalizia mchezo aliokwisha anza ingawa uligharimu maisha yake gerezani alirudi na suluhisho la kusameheana na akagundua hawezi kendelea kuwa rais hivyo akaongoza kwa kipindi kimoja na hakuweza kuendelea kwenye uchaguzi uliofuata.

Alivyoweza kumalizia ndiko kumempa heshima mpaka leo ambayo hutaweza kuiondoa hata kama unajua madhaifu yake kwa kiwango kikubwa sana.

Haina haja ya kulazimisha heshima bali kitakachokufanya uheshimike ni namna ambavyo unamalizia mambo yako. Ndio maana katika mashindano ya michezo mbalimbali hata kama ukimfunga mtu magoli mengi na mwisho wa siku ukashindwa kufika fainali na pengine uliyemfunga ndio amechukua kombe wewe hauna kitu cha kujivunia kwakuwa haujaweza kumaliza vizuri. Unaweza ukaongelea jinsi mambo yalivyokwenda na namna ulivyomfunga bali hauna kombe, sherehe mtaa wa pili.

Katika kila jambo tunalolifanya inatubidi kuangalia je tunamaliziaje suala hili? Je biashara yako inamaliziaje utoaji wa huduma? Je mipango yako huwa unaimaliziaje? Na kama wewe ni msanii je unapanga kumalizia vipi? kwanini wengine wanashindwa kumalizia vizuri? Tatizo ni nini hasa?

Kama mwanadamu unaweza kuwa na nafasi kubwa na kwa kipindi fulani ukajiona uko juu, ukasahau kwamba kuna siku unatakiwa kushuka. Ukijua hivyo utaweza kujipanga na kuandaa umaliziaji wako pasipo kupoteza heshima yako. Mara nyingi umaarufu unaturewesha kiasi kwamba tunasahau kwamba kuna siku tunatakiwa kumalizA na kutoka au kutakuja mtu maarufu kuliko wewe mwenyewe. Unatakiwa kumalizia vyema mambo yako ili kujenga heshima yako.

Related Articles

Bongo5

FREE
VIEW