Umoja wa Mataifa aitaka Zimbabwe itangaze haraka matokeo ya uchaguzi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon tarehe 7 alitoa taarifa ikieleza kufuatilia kutotangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais baada ya uchaguzi wa urais wa Zimbabwe kufanyika siku 9 zilizopita

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki-moon tarehe 7 alitoa taarifa ikieleza kufuatilia kutotangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais baada ya uchaguzi wa urais wa Zimbabwe kufanyika siku 9 zilizopita.

Taarifa hiyo iliihimiza kamati ya uchaguzi ya Zimbabwe itekeleze jukumu lake, kuhakikisha uwazi wa uchaguzi na kutangaza haraka matokeo ya uchaguzi huo. Taarifa hiyo ilizitaka pande husika zichukue hatua kwa kutekeleza majukumu yao, kuvumilia zaidi, kutatua masuala yote yanayohusu uchaguzi huo kupitia kwa njia ya mazungumzo, ili kuhakikisha maslahi ya wananchi wa Zimbabwe.

Mwishoni mwa mwezi Machi, Zimbabwe ilifanya uchaguzi wa pamoja wa urais na wa bunge kwa mara ya kwanza. Mpaka sasa kamati ya uchaguzi imetangaza matokeo ya uchaguzi wa baraza la juu, lakini matokeo ya uchaguzi wa urais ambayo yanafuatiliwa kabisa bado hayajatangazwa, hayo yanasababisha migongano kati ya chama cha tawala na chama cha upinzani.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents