Habari

Umoja wa Mataifa haki za binadamu walaani ubaguzi Marekani

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu ametoa wito wa kuchukuliwa hatua za haraka na za kina kupambana dhidi ya ubaguzi wa kimfumo nchini Marekani.

UN Commissioner Michelle Bachelet honors journalists | DW News - latest  news and breaking stories | DW | 03.05.2020

Michelle Bachelet pia ameihimiza Hong Kong kufuatilia kwa karibu utekelezaji wa sheria ya usalama wa kitaifa nchini China iliyolalamikiwa vikali na wanaharakati wengi.

Kauli ya Bachelet imetolewa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa hivi karibuni wa baraza la haki za binadamu linaloungwa mkono na Umoja wa Mataifa.

Kamishna Mkuu huyo wa shirika la Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu pia ameelezea wasiwasi wake juu ya hali ya haki za binadamu nchini Myanmar, Nicaragua, Venezuela miongoni mwa sehemu nyengine.

How to cope with President Trump Stress Disorder - New York Daily News

Pia ameonyesha wasiwasi wake juu ya utumiaji wa nguvu kupita kiasi wa polisi katika visa kama vile kupigwa risasi kwa Jacob Blake mjini Kenosha, Wisconsin mwezi uliopita, na ufichuzi wa maelezo ya kina kuhusu kifo cha Daniel Prude, mjini Rochester, New York mapema mwaka huu.

Amesema ukosefu wa uwajibikaji katika matukio mengi ya mauaji huko nyuma unatilia mkazo uzito wa mzozo huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents