HabariUncategorized

Umoja wa Mataifa wataka Saudi Arabia iwajibishwe Kwa kukubali mwandishi Khashoggi aliuawa ndani ya Ubalozi wao

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa wataka Saudi Arabia iwajibishwe

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres, mashirika ya kutetea haki za binadamu na vyama vya waandishi wa habari vimetaka waliohusika na mauaji ya mwandishi habari Jamal Khashoggi nchini Uturuki
waadhibiwe.

Guterres amesema amepata wasiwasi mkubwabaada ya Saudi Arabia kukiri kuwa Khashoggi alifikwa na umauti kwenye ubalozi wake mdogo. katibu mkuu wa Umoja wa mataifa  ameongeza kusema kuwa kuna haja ya kufanyika uchunguzi wa haraka na wa kina kuhusiana na kadhia hiyo ili waliohusika wachukuliwe hatua. Uturuki imeelezea kutokufurahishwa nanhatua ya Saudi Arabia ya kuchelewa kukiri kwamba imehusika na mauaji ya Khashoggi na kukitaja kitendo hicho kuwa cha kufedhehesha.

Shirika la Amnesty International limesema maelezo ya Saudi Arabia kuhusu mauaji ya Khashoggi yanaonekana kufunika mauaji ya kinyama,na taarifa nyingine mbaya zinazodhihirisha  kwamba Saudi Arabia inakiuka haki za binadamu. Shirika hilo la Amnesty International limeitaka nchi hiyo kuutoa mwili wa mwandishi huyo wa habari ili ufanyiwe uchuguzi kubainisha chanzo cha kifo chake.

Taarifa ya vyombo vya habari vya serikali nchini Saudi Arabia imeongeza kusema kuwa mshauri wa mahakama ya Saudi Arabia, Saud al-Qahtani na naibu Mkuu wa idara ya upelelezi Ahmed Asiri wamefukuzwa kazi.

Trump aikingia kifua Saudia Arabia

Kabla ya Saudi Arabia kutoa taarifa hiyo, rais wa Marekani Donald Trump alisema anaweza kuzingatia kuiwekea vikwazo Saudi Arabia lakini wakati huo huo amesisitiza umuhimu wa uhusiano wa nchi hizo mbili. Trump amesema maelezo yaliyotolewa na Saudi Arabia ni ya kuaminika.

Chanzo DW Swahili

By Ally Juma

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents