Burudani

Video: Umoja wa Ulaya watoa shavu kwa vijana

Umoja wa Ulaya na washirika wake tokea nchi ya Uholanzi, Ubalozi wa Ufaransa,Alliance Francaise pamoja na British Council kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania rasmi wamezindua shindano la utengenezaji filamu kwa vijana kuanzia umri wa miaka 18-35.

Akizindua shindano hiyo Jumatatu hii, Bi Susanne Mbise – Afisa habari wa Umoja wa Ulaya, amesema shindano la European Youth Film Competition 2017, litawapatia nafasi vijana kuweza kukutana pamoja na kujadili mambo kadhaa ikiwemo mabadiriko ya tabia ya nchi.

Alisema washiriki watakaoweza kuchaguliwa katika shindano hilo watapata elimu kwenye warsha itakayoandaliwa ili kuweza kujua juu ya utengenezaji wa filamu kwa kukutanishwa na mmoja wa waandaji wa makala ya “Tapis Rouge” aitwaye Kantarama Garighiri tokea nchini Ufaransa.


Washiriki hao watatakiwa kutengeneza filamu fupi ya dakika 5 mpaka 10, na itausisha vijana wa Kitanzania pekee (Bara na Kisiwani).

Jumla ya kiasi cha shilingi milioni 15 zitatolewa, ikiwa ni milioni 7 kwa mshindi wa kwanza, mshindi wa pili milioni 5 na mshindi wa tatu milioni 3.

Naye mratibu wa shindano hilo kutoka Andreson Media, Musa Sakari, amesema kuwa hili ni shindano la kwanza kufanyika Tanzania, na kwa zaidi ya miaka 25 wamekuwa wakiandaa matamasha ya kutazama filamu nchini na wameona sasa kuna umuhimu wa vijana kuweza kushiriki katika mashidano hayo.

“Tunahitaji kizazi kipya katika utengenezaji wa filamu nchini, ukizingatia soko la filamu limeshuka hivyo vijana ni wakati wao kuweza kuonyesha ujuzi katika filamu,” amesema Afisa mawasiliano na uhusiano Bodi ya filamu nchini Abuu Kimario.

Fomu za kuweza kushiriki zinatolewa Alliance Francaise, British Council na Bodi ya filamu nchini, ambapo utowaji wa fomu utahitimishwa ifikapo Juni 4 mwaka huu. Na washiriki 30 watakao patikana wataweza kupatiwa mafunzo kuhusu filamu, na ifikapo Septemba mwaka huu filamu zilizo shinda zitaanza kutazamwa katika tamasha jijini Abuja na baadae zitaoneshwa Alliance Francaise, British council na online.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents