Habari

UN wataja mataifa 38 yanayoiabisha Dunia, Afrika Mashariki yatoa nchi moja

Umoja wa Mataifa Jumatano hii umetaja mataifa 38 “yanayo aibisha” yakiwemo China na Russia kwa kile walichodai kuwa ni ulipizaji kisasi au vitisho dhidi ya wale wanaoshirikiana na umoja huo kwa ajili ya kuchunguza ukiukaji wa haki za binadamu.

Miongoni mwa unyanyasaji ulotajwa ni pamoja na mauaji, mateso na kukamatwa kiholela kwa watu hao.

Ripoti ya kila mwaka iliyotolewa na Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres imetaja pia kuwepo na kampeni kuwafuatilia, kuwatendea maovu, na kuwaaibisha hadharani watetezi wa haki za binadam na waathiriwa.

Mataifa hayo 38 yanajumuisha 29 yenye kesi mpya na mengine 19 yakikabiliwa na kesi zinazoendelea.

Ripoti inaeleza kwamba mataifa mengi yanadaiwa kuwafungulia mashtaka wanaharakati wa haki za binadamu kwa ugaidi au kushirikiana na mataifa ya kigeni kuhujumu hadhi na usalama wa taifa, ikiwa ni njia ya kuwatishia wasiendelee kushirikiana na UN katika uchunguzi huo.

Kesi hizo mpya zinazochunguzwa ziko Bahrain, Cameroon, China, Colombia, Cuba, DRC, Djibouti, Misri, Guatemala, Guyana, Honduras, Hungary, India Israel, Krygyszstan, Maldives.

Nyingine ni Mali, Morocco, Myanmar. Ufilipino, Rwanda. Saudia Arabia, Sudan Kusini, Thailand, Trinidad na Tobago, Uturuki, Turkmeni na Venezuela.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents