Habari

UN watoa tahadhari ‘Ongezeko la joto duniani tishio kwa maisha ya binadamu’ (Video)

Umoja wa Mataifa umeonya kuwa ongezeko la joto sasa ni tishio kwa binadamu kuliko ilivyokua huko miaka ya nyuma.

Akizungumza katika mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya hali ya hewa huko Poland, kiongozi wa Umoja wa Mataifa kuhusu hali ya hewa, amesema kuwa mwaka huu ni miongoni mwa miaka minne yenye joto zaidi duniani.

Wawakilishi kutoka sehemu mbalimbali duniani wanatarajia kuleta mabadiliko kwa kuanza kufanyia kazi mkataba wa hali ya hewa wa Paris.

Aidha, rais wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya hali ya hewa, Maria Esposa amesema kuwa jitihada za haraka zinahitajika kuchukuliwa, huku benki ya dunia, ikitoa dola bilioni 200 zilizoelekezwa kwa nchi zinazochukua hatua za kupambana na mabadiliko ya tabia nchi kwa miaka mitano ijayo.

Hata hivyo, viongozi wa nchi 29 wanatarajiwa kuhudhuria, kwa upande wa China na Umoja wa Ulaya wanatarajiwa kuonyesha kuwa kuna uwezekano wa ushirikiano wa pamoja hata katika kipindi hiki cha uongozi wa Donald Trump nchini Marekani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents