Habari

UN yaitaka Dunia kupinga vita baridi vya Marekani na China

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameitolea wito dunia kusitisha vita baridi kati ya Marekani na China, na kusimamisha mizozo ili iweze kujikita katika mapambano dhidi ya janga la COVID-19.

UN chief warns over threat of new Cold War between US and China | Euronews

Guterres amesema dunia inachukua mwelekeo wa hatari sana, na kuonya kuwa haiwezi kuhimili mustakabali ambapo mataifa mawili yanayoongoza kiuchumi yanaigawanya dunia, kwa kila upande kuweka sheria zake za kifedha na za kibiashara.

Katibu mkuu huyo amesema kinachohitajika sio serikali ya dunia, bali mazingira mazuri ya uongozi. Guterres ameendesha kampeni ya kumaliza mizozo yote ya kivita duniani ili kupambana na janga la virusi vya corona, na ameitaja baadhi ya mifano ya mafanikio katika juhudi hizo, ikiwemo usitishwaji wa mapigano nchini Cameroon na Colombia.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents