Unasoma kwa Malengo?

Unasoma kwa Malengo?
Wengi wetu tunajua umuhimu wa elimu. Tupo tulioenda shule, tupo tuliopita shule, tupo tulioingia madarasani, tupo tuliokwepa umande… alimuradi tu, tupo wa aina kibao. Hata hivyo, licha ya kutofautiana kote huko, wote kwa pamoja tunaamini na kujua kuwa elimu ndio ufunguo wa maisha. Lakini swali moja ambalo pengine wengi wetu huwa hatujiulizi ni hili; Je, tunasoma ili iweje hasa?

Wengi bilashaka watasema ili waweze kuwa na maarifa ya kujiendesha kimaisha na majibu mengine mengi ya aina hiyo.

Swali jingine linakuja hapo hapo; Je, huwa tunasoma kwa malengo? Jibu la swali hili bilashaka ni tete kidogo, maana ukweli ni kwamba wengi wa sisi Watanzania, ni watu ambao tumekuwa tunaenda shuleni au chuoni kwasababu tu tumepata nafasi ama kwasababu tumekosa kitu Fulani tulichokuwa tukitaka.

Katika mkondo huu ndio tunapokutana na kundi la watu ambao katika maisha yao walitamani au kuwa na ndoto ya kuwa akina Fulani, lakini wakashindwa na kuamua kuchukua njia nyingine si kwasababu ya kupenda, bali kwasababu tu ya kukosa malengo na uelekeo wa umakini.

Je, hicho unachosoma wewe, ulishakipigia mahesabu na kujua kitakulipa kwa kiasi gani? Je, ni taaluma zipi ambazo hulipa sana?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents