Habari

Unataka kufanikiwa? Acha kufanya mambo haya

Mambo ni rahisi sana kwa uhakika kama unataka kufikia mafanikio makubwa kwa kile unachokifanya. Haya ni mambo ambayo kama unataka mafanikio ni lazima uyaache mara moja.

41854

1. Kupuuzia Mambo

Hapa tunazungumzia kupuuzia mambo ya msingi au matatizo au ishu ambazo ni za aibu unazotamani kujificha chini ya uvungu wa kitanda. Kuna mtu mmoja aliwahi kusema tabia mbaya huendelea kukua na kuongezeka kulingana na umri.

Kwa bahati mbaya kuna watu hawawezi kasi ya  maisha ya sasa na hivyo kushindwa kushughulikia matatizo yanayoambatana nayo kwa kuyapuuza na kufikiri kwamba yataisha yenyewe. Kwa sasa huwezi ukapuuzia nguvu ya teknolojia na ukafikiri kwamba unaweza kufanikiwa zaidi ya hapo bila kuwekea mkazo teknolojia iliyopo sokoni. Na kama una tabia mbaya wala huishughulikii haitakufanikisha bali itakuyumbisha na kukuondolea mafanikio yako kabisa.

2. Kuwa na Wivu

Watu  ambao hawana mafanikio ni wenye wivu mkubwa sana na mara nyingi huwa hawafurahii wengine wakifanikiwa hivyo hushindwa kuchukua wajibu wao wa kushindwa kuweka juhudi katika wanalolifanya kwenye maisha yao. Watu wenye wivu hutafuta namna ya kuwashusha wenzao waliofanikiwa na wakati mwingine huwa sababu ya kuwekea vikwazo wanzao ili wasiweze kufanikiwa.

3. Wivu husababisha uchungu

Watu wenye wivu hutengeneza uchungu fulani dhidi ya yule aliyefanikiwa. Watu wengi ambao hawajafanikiwa kimaisha / kitaaluma na hata kibiashara huweka hasira kwa mtu mwingine badala kushughulikia maisha yake au taaluma yake mwenyewe. Kutokana na hali hiyo mtu huyo huwa hawezi kutoa ushirikiano kwa wengine, na ni moja ya watu ambao huwa wako tayari kumharibia mwenzake kazi au biashara kutokana na hali hiyo.

4. Uvivu na kutojituma

Kutokana na kuwa na wivu na uchungu kwa wengine watu ambao hawajafanikiwa huona shida kufanya kazi na wengine hivyo huwa wavivu na kuacha kujihusisha kwa juhudi kwenye kazi kama wengine ili tu asione watu wakisogea au kufanikiwa. Hufanya kazi kwa taratibu sana kiasi kwamba matokeo au muda uliotarajiwa kukamilisha kazi hushindwa kufikiwa mapema.

5. Kupenda kujificha wakati wa kazi

Watu ambao hawajafanikiwa kifikra na kwenye maisha wanakuwa na tabia ya kukimbia au kujificha ili wasipewe majukumu au kuongezewa majukumu. Hii unaweza kuwa ulishakutana na watu ambao wanatumwa kufanya kazi sehemu fulani na kwa bahati nzuri kazi hiyo ikafanikiwa kuisha mapema, watakachokifanya ni kusema kwamba bado wanaendelea na kazi ili isijulikane kwamba kazi imekwisha ili waweze kwenda kumhudumia mteja mwingine.

8. Kutia aibu watu wengine

Kwa sababu hawa watu wanakuwa hawajiamini hivyo wanachofanya ni kujaribu kuwaaibisha watu wengine. Hupenda kuwa katikati ya watu wanaofanya sana kazi ili kuweza kuwadhalilisha wale wengine kwa kujaribu kuwachafua au kuwadhalilisha kwamba wana utendaji mbovu. Ukweli wanajaribu kupambana na ukosefu wa kujiamini ndani yao wenyewe.

9. Kutumia muda mwingi kwenye mitandao ya Kijamii

Hawa watu wanaitwa walevi wa mitandao, kama uliwahi kuona watu ambao muda wote wanatumia kwenye televisheni  bila kuchoka. Vile vile na watu ambao hawajafanikiwa na wala hawataweza kufanikiwa wanatumia muda mwingi mwenye mitandao bila kufanya kitu cha maana. Muda wanaotumia kwenye mitandao hawajui kwamba unaingiliana na malengo na utendaji kazi zao kwenye maisha yao binafsi.

10. Usumbufu wa chini chini  na Usaliti

Tabia hii inakubidi uweke kichwani mwako wakati mwingine unapohisi kusalitiwa na mtu, je ulishawahi kupitia hali ya kwamba mlikuwa mnajaribu kufanya jambo pamoja halafu jambo limepotea juu juu au kujikuta limefanyika sehemu nyingine kabisa bila ya wewe kujua? Ukweli watu ambao hawana furaha na hawajafanikiwa hawatapenda kuona umefanikiwa hivyo wakati mwingi watataka kusaliti mipango na miradi yako ili usifikie malengo huku wakija na sababu lukuki kwanini imetokea hivyo.

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents