Habari

Unataka kupandishwa cheo? Haya ni mambo ya kuzingatia kwanza

Wakati unasubiri kupandishwa cheo au kupandishwa daraja, unahitaji kujua vitu vya kufanya ili vikusaidie kwenda ngazi nyingine bila kutumia nguvu na kupambana na mabosi wako.

1017697_634994306519488_1432148397_n
Credits: OGS Studios

1. Kama unalipwa kidogo, wewe fanya zaidi

Watu ambao wako nafasi za chini wengi wao hukwepa kazi za kufanya. Wanataka kufanya kile tu waliajiriwa kufanya, na hushangaa kwanini hawapandishwi daraja au cheo. Napenda kukushauri kwamba hata kama jambo ambalo unaweza kufanya haliko kwenye majukumu yako jaribu kuona unaweza kusaidia kwa namna gani. Fanya kwa uangalifu mkubwa bila kuleta mzozo usiokuwa wa lazima hapo kazini. Mtafute kiongozi wako au msimamizi wako wa kazi kwa jinsi gani unaweza kuingia kwenye kazi fulani na kuweza kusaidia kama kuna ulazima. Ongea na mtu sahihi na jaribu kusaidia sehemu sahihi ambayo utaifanya kwa ufanisi mkubwa.

2. Uwe Mjasirimali wa ndani

Mjasiriamali wa ndani ni mtu anayetumia akili za kijasiriamali, uhusiano, ujuzi na tabia yake  ndani ya kampuni fulani kutengeneza kitu kipya, wazo jipya kwa ubunifu mpya kuleta bidhaa na huduma mpya. Iwe unatengeneza wazo jipya la kampuni katika kusaidia na kuhusiana na jamii, kuinua vipaji, jukumu lako ni kuhakikisha hilo jambo linafanikiwa. Kama unafungua kitengo kipya kuna uwezekano wa wewe kuwa bosi wa hicho kitengo na ukifanikiwa unakuwa na uzoefu mkubwa wa kiuongozi.

3. Pata mtandao wako wa ndani na uendelee kufanya kazi

Ni vizuri kutengeneza uhusiano na watu vizuri kwenye idara yako na kama timu ndani ya kampuni yenu. Nimeona wafanyakazi wengi hawaendi juu hata hawafahamiani vizuri zaidi na wafanyakazi wenzao, jaribu kuwafahamu wafanyakazi  wenzako kwani unaweza kupata fursa kwao na kukusaidia kwenda viwango vingine.

4. Linganisha malengo yako ya muda mfupi na muda mrefu

Unapoangalia malengo yako, jaribu kuangalia malengo ya muda mfupi na malengo ya muda mrefu. Unatakiwa kujua malengo ya idara yako ya muda mfupi na muda mrefu ili uweze kufanya kazi na Bosi wako kwa mwelekeo wa kampuni.

5 Acha Kulalamika

Watu wengi hupenda kufanya kazi na watu wenye furaha, lakini sehemu nyingi za kazi leo kuna walalamikaji wengi sana. Mabosi wa juu hupenda kufanya kazi na watu wanaoona fursa na wenye ujuzi badala ya watu ambao hulalamika kwenye kazi. Kulalamika kunapoteza hali ya kufanya kazi, endapo unafanya kazi na mtu mlalamishi hawezi kukusaidia kupata ufumbuzi wa jambo au tatizo hapo kazini. Tazama zaidi fulsa wakati wote unapofanya kazi.

6. Uliza

Kuuuliza ni jambo la kawaida , sijui ni watu wangapi wanajua kuna nafasi gani zipo wazi kwenye makampuni yao. Ongea na bosi wako ambaye unajua anaweza kukuelewa na kukwambia kampuni inataka nini, wanaume huuliza kirahisi kuliko wanawake. Kama una uwezo na uzoefu wa vitu ambavyo umeendelea kufanya kwenye kampuni hiyo, unapaswa kujua uzoefu gani unahitajika katika nafasi hiyo mpya na wewe onyesha uzoefu wako na kwamba unaweza kuchukua hiyo nafasi.

Pata ushauri na ujiandae kwa kwenda viwango vingine kikazi.

 

 

Awali Mwaisanila

A Personal Career Development specialist, passionate about empowering emerging generations of student, graduates and working class.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents