Burudani

‘Unaweza kujiita mkali wa kuvaa kumbe sio’ – Chibwa

Msanii Chibwa wa Tanchy anayefanya vizuri na wimbo ‘Unamtambia Nani’, amefunguka na kusema si vizuri kwa wasanii kuwa na mtazamo wa jumla kuhusu jambo fulani kama mavazi na kuchukua mtazamo huo kama ni sehemu ya wasanii wote wakati kila mmoja ana mtindo wake maisha katika uvaaji.

Chibwa

Kauli ya Chibwa inakuja mara baada ya msanii kutoka Tip Top Connection, Dogo Janja kudai yeye ndiye msanii ambaye kwa sasa anaongoza kuvaa hapa Bongo. Chibwa amesema kwenye mavazi kuna ile mtu unapenda kuvaa nini  na wewe unajikubali kwa kile unachokivaa  na washikaji zako wale ambao unakutana nao wanakupa big up kwa vile ulivyo.

“Lakini tabia ya mtu mwingine na watu wengine wewe hutakiwi kuijudge, kwa hiyo wewe huwezi kuwa judge wa watu wengine wote kwa kusema wewe ni mkali wa kitu fulani wakati watu walio chimbo wakikuangalia wanaona mbona mdogo wetu kama unataka kuparamia miti mikubwa,” asema hayo katika kipindi cha Daladala Beats cha Magic FM.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents