Habari

Unazifahamu project Mbili Za Akon Za kusaka Vipaji Vipya


Msanii Aliaune Thiam ambaye anajulikana zaidi kama Akon ameanzisha project mbili za muziki katika kusaka vipaji ambavyo atavibadilisha na kuwa vya kimataifa. Moja kati ya project hizo ni Akonic ikiwa na maana ya kusaka vipaji vya ki Afrika na kuviendeleza ili kuvifikisha katika next level ya usupa star wa kidunia.
Tayari msanii huyo na mshirika wake Nickie Shapira ambao kwa pamoja ni wakurugenzi wa project hiyo wameshapata project ya kwanza ambayo imeshafanyika nchini DRC Congo na kupata udhamini wa kampuni ya simu ya Vodacom na kupewa jina la Vodacom Super Star ambalo ni shindano la kusaka vipaji kwa staili ya Bongo Star search kama BSS.
Project hiyo tayari imeshazaa matunda ambapo zao la kwanza la mradi huo nchini DRC Congo msanii Sarah Kalume amekuwa mshindi wa kwanza katika shindano hilo na kupata nafasi ya kufanya kazi na Akon ambayo imepewa jina la light Switch.
Project nyingine inaitwa HitLab ambayo nayo ni ya kusaka vipaji dunia nzima kwa wasanii kutuma nyimbo zao kwenye anwani ya mtandao www.hitlab.com alafu wanapigiwa kura na wananchi na msanii ambaye nyimbo zake ama nyimbo yake ikipata kura nyingi zaidi anapata nafasi ya kuingia studio za Akon ambazo amezibatiza jina la Akon HitLab na kupata mkataba wa kumuendeleza.
Haya sasa wasanii wa kibongo tumieni nafasi hiyo.
Tizama Video ya wimbo Light switch Sarh Ft Akon

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents