Habari

Under the Spotlight: Osse Sinare – ‘Ushindani si tishio, ni motivation’ Kalikawe – Passion kwanza pesa baadaye, utafanikiwa’

Ijumaa iliyopita, (28 February) Ndovu Special Malt waliandaa mjadala wa ‘Under the Spotlight’ unaofanyika kila baada ya miezi kadhaa katika mwaka kuwamulika vijana wa Kitanzania wanaofanya vizuri kwenye fani mbalimbali.

Brand Manager
Meneja wa bia ya Ndovu, Pamela Kikuli

Awamu hii mjadala huo uliofanyika New Africa Hotel jijini Dar es Salaam, ulimhusisha mpiga picha maarufu kwa sasa kutokana na ubora wa kazi zake, Osse Greca Sinare wa OGS Studios, pamoja na mbunifu wa mavazi na urembi wa ndani ya nyumba (Fashion and Interior Designer) Kemi Kalikawe.

Osse ambaye amekuwa akifanya kazi ya upigaji picha professional na makampuni mbalimbali nchini, alisema kwake ushindani si tishio, bali ni kitu kinachompa msukumo wa kujituma zaidi.

Osse
Osse Sinare

“Kitu kimoja ambacho nakiona hapa Tanzania ni kwamba siku zote watu huhofia ushindani na sioni kama kuna sababu ya kuogopa ushindani. Ushindani unatakiwa kuwa ‘kuna huyu mtu mwingine anafanya mradi huu mzuri’ unakubali, unampongeza na unawafanya watu wajue na kisha unarudi kwenye ubao wa kujipanga na kusema ‘nini nachotakiwa kukiweka mezani’. Ukiona ushindani ufanye kama kitu kinachokupa msukumo wa kufanya kazi nzuri zaidi,” alisema Osse.

Kwa upande wake Kemi Kalikawe ambaye kazi moja wapo anayofanya ni kuwavisha waigizaji wa tamthilia ya Siri ya Mtungi, Kemi aliwashauri vijana wanaotaka kuingia kwenye tasnia ya ubunifu kutoweka mbele pesa kwakuwa pindi wakikutana na ugumu watashindwa kuvumilia.

Kalikawe
Kemi Kalikawe

“Kama pesa ndio inakupa msukumo wa kazi utajikuta ukiacha kila unachofanya. Kama ni kitu unachokipenda (passion) utaendelea kuifanya na kila kitu kitakaa sawa,” alisema. Kalikawe aliongeza kuwa internet ni kila kitu kinachoweza kumpa elimu mtu yeyote atakayependa kujifunza na kuwa mtu kusoma au kuishi nje ya nchi si kigezo cha yeye kufanikiwa akirejea nchini.

“Unaweza kuwa nje na uzoefu utakaoupata usikusaidie chochote unachokuja kukifanya mwishoni. Lakini inakupa uwezo wa njia tofauti ya kufikiria kwasababu umekaa na watu tofauti, umeona vitu tofauti. Unaweza kufanya hapa hapa (Tanzania), suala la kusafiri na kwenda sehemu zingine ni kwenda tu kuona watu tofauti huko,” alisema.

Naye Osse aliyechukua masomo yake ya chuo kikuu nchini Malaysia, alisema kuwa changamoto za kazi ni zile zile haijalishi ukiwa Tanzania ama nje ya nchi. “Ni kujituma kwako tu ndio kunaweza kukusukuma na kufanikiwa ukilinganisha na mwingine yeyote. Kila mtu anasema ‘walienda kusoma nje ya nchi’, hapana sio hivyo. Una internet, hakuna kisingizio chochote unachoweza kukitumia.”

Hata hivyo, Kemi anasema nguo nyingi anazozitengeneza hununuliwa zaidi na raia wa nchi za nje ama Watanzania walioishi nje ya nchi kuliko Watanzania wa kawaida.

“Kwangu mimi nadhani si sababu ya bei,” alisema Kemi. “Kwasababu ukiangalia bei za vitu kwenye maduka ambako unapata bidhaa zilizotengenezwa China, unapata kila duka lina vitu vilevile lakini bei ya nguo zake ni sawa na hizo tu. Kwangu nahisi tatizo ni kukubalika. Wanaweza kuiona nguo na wakaipenda lakini wanaweza kwenda kwa fundi cherehani na kuitengeneza wenyewe. Ofcourse, mimi nitatoza zaidi kuliko fundi cherehani sababu mimi ni mbunifu namlipa fundi atengeneze nami natakiwa kupata faida.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents