Habari

Unene wa kupitiliza wamkosesha Viza ya kuishi New Zealand mwanaume kutoka Afrika Kusini

Mwanaume mmoja raia wa Afrika Kusini amejikuta akinyimwa Viza ya kuishi nchini New Zealand kutokana na kuwa mnene wa kupitiliza.

albert-2

Kwa mujibu wa taarifa ya BBC maafisa wa utawala nchini New Zealand wamemwambia mwanamume huyo aitwaye Albert Buitenhuis ambaye pia ni mpishi kuwa ni mnene kupita kiasi kuweza kuruhusiwa kuishi nchini humo. Maafisa hao walisema kuwa Buitenhuis, mwenye uzito wa kilo 130 hana afya nzuri.

Bwana Buitenhuis na mkewe walihamia nchini New Zealand mwaka (2007). Wakati huo mwanamume huyo alikuwa na uzito wa kilo 160 kiasi ambacho amefanikiwa kupunguza kilo 30 na kuwa 130 ambazo hata hivyo bado haijamsaidia kuruhusiwa kuendelea kuishi nchini humo.

albert
Albert na mkewe

“Tumekuwa tukiomba viza hizo kila mwaka na hapajawahi kuwa na matatizo yoyote,hawajawahi kuzungumzia uzito wa Albert wala afya yake wakati hata alipokuwa mnene kushinda sasa.”alisema mke wa Albert.

Lakini mapema mwezi Mei, wanandoa hao waliambiwa kuwa hawatapokea visa mpya kwa sababu ya unene wa bwana Buitenhuis.

“nimeshangazwa sana kwa sababu kwa sasa ameweza kupoteza kilo 30 tangu tuje hapa New Zealand, ” alisema mkewe Buitenhuis.

Wawili hao wamemuomba waziri wa uhamiaji wa nchi hiyo kuwaruhusu waendelee kuishi nchini humo kwani bwana Buitenhuis ameweza kupoteza kilo.

Msemaji wa uhamiaji alisema kuwa bwana Buitenhuis alinyimwa visa mpya kwa sababu ya tisho kwa afya yake kutokana na uzani wake, kuwa anaweza kupatwa na kisukari, shinikizo la damu na maradhi ya moyo.

New Zealand ni mojawapo ya nchi zenye idadi kubwa ya watu wenye unene kupita kiasi huku takriban asilimia 30 ya watu wake wakiwa waathiriwa.

SOURCE: BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents