MichezoUncategorized

United yapigwa kipigo kizito Old Trafford vijana wa Spurs wakitakata

Klabu ya Manchester United imeshindwa kutamba kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Old Trafford baada ya kujikuta ikipokea kipigo cha jumla ya mabao 3 – 0 dhidi ya Tottenham Hotspur mchezo uliyopigwa usiku wa Jumatatu.

 Katika mchezo huo uliyokuwa na ushindani mkubwa umeshuhudia vijana wa Jose Mourinho wakipokea kipigo hicho kutoka kwa Spurs kupitia kwa wachezaji wao, Harry Kane akifunga dakika ya 50 huku kijana Lucas Moura akifunga mawili dakika ya 52 na 84.

Kikosi cha Man Utd: De Gea (5), Valencia (5), Shaw (5), Jones (4), Smalling (4), Matic (4), Fred (5), Herrera (5), Pogba (4), Lingard (5), Lukaku (5).

Wachezaji wa akiba :Sanchez (5), Lindelof (4), Fellaini (5)

Kikosi cha Tottenham: Lloris (7), Trippier (7), Rose (6), Alderweireld (7), Vertonghen (7), Dier (6), Dembele (7), Alli (6), Eriksen (7), Moura (9), Kane (8).

Wachezaji wa akiba :Aurier (NA), Davies (NA), Winks (NA)

matchMchezaji bora wa mechi hiyo ni Lucas Moura ambaye amefanikiwa kufunga jumla ya mabao mawili peke yake.

Mpaka sasa United imepoteza jumla ya michezo miwili kati ya mitatu iliyocheza tangu kufunguliwa kwa pazia la ligi kuu msimu huu.

Hii ni kwa mara ya kwanzaa kupoteza michezo miwili kati ya mitatu ya ufunguzi tangu mwaka 1992.

Related Articles

2 Comments

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents