Soka saa 24!

UNYAMA: Baba aua mwanae kwa malipo ya Tsh. mil 5

Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linwashikilia watu wawili kwa tuhuma za mauaji ya mtoto, Rose Japhet (6), aliyeuawa Kijiji cha Msewe Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya kutokana na imani za kishirikina.

Akizungumza na wandishi wa Habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, Ulrich Matei amesema watuhumiwa walimuua mtoto huyo Mei 3, 2019 mwaka huu kwa kumnyonga kisha kumnyofoa baadhi ya viungo.

Aliwataja wanaoshikiliwa kuwa ni Andrew Mwambuluma mkazi wa Mbalizi ambaye pia ni mmiliki wa shule ya Sekondari Ushindi na baba mzazi wa marehemu, Japhet Nguku (37) mkazi wa Kijiji cha Msewe wilayani Mbarali.

Kamanda Matei amesema mwili wa mtoto huyo ulikutwa umetelekezwa kwenye msitu wa Hifadhi wa Chimala wilayani Mbarali ukiwa umekatwa kanyagio la mguu wa kulia na baadaye ilibainika kuwa kanyagio hilo lilikuwa limefukiwa Mbalizi.

Akielezea chanzo cha tukio hilo, Kamanda Mtei amesema ni tamaa ya fedha ambapo mzazi wa mtoto huyo, Japhet alikubali kumuuza mtoto wake kwa mmiliki wa shule ya Ushindi kwa shilingi milioni 5 ili achukuliwe viungo na kwenda kutengeneza ndagu za biashara.

Japheti alikubali kumtoa mtoto wake kwa Andrew ambaye ni mfanyabiashara wa shule ya Sekondari ili akatwe kanyagio la mguu wa kulia kwa ajili ya kupeleka kwa mganga wa kienyeji ili atengenezewe ndagu (dawa ya utajiri) kwa ajili ya kuendesha biashara zake,” amesema Kamanda Matei.

Alisema baada ya Japhet kukamatwa na kubanwa alieleza ukweli wa tukio hilo ambapo ilibainika kuwa kanyagio la mtoto huyo lilikuwa limewekwa kwenye karatasi ya plastiki, kisha kufukiwa Mbalizi umbali wa zaidi ya kilomita 70 kutoka eneo alipouawa.

Baada ya mmiliki wa shule kutajwa kuhusika na tukio hilo, alikamatwa na alipohojiwa alikiri kuhusika kisha wawili hao wakapelekwa mahabusu wakati uchunguzi unaendelea kufanyika ili kubaini ukweli zaidi,” alisisitiza Kamanda Matei.

Kamanda Matei alisema kwa sasa Jeshi hilo linaendelea na ufuatiliaji wa tukio hilo ikiwa ni pamoja na msako wa kumtafuta mganga ambaye alikuwa anashirikiana na wauaji hao.

Chanzo: Mtanzania

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW