Habari

Unyama uliofanyika Kampala

Watu zaidi ya 60 wameuawa katika milipuko miwili iliyotokea kwenye mji mkuu wa Uganda, Kampala wakati wakiangalia mechi ya fainali ya mpira wa miguu ya Kombe la Dunia usiku wa juzi. Haijajulikana mpaka sasa milipuko hiyo imesababishwa na nini, lakini polisi wamesema ilitokea kwenye klabu ya mchezo wa raga na kwenye mgahawa wakati mashabiki wakiangalia mechi hiyo baina ya Hispania na Uholanzi.

Inspekta wa Polisi Kal Kayihura alisema mabomu hayo yalikuwa yakilenga watu waliokusanyika kuangalia Kombe la Dunia.

Kayihura alisema kwamba polisi anaamini kundi la wanamgambo la al-Shabab linahusika na shambulio hilo. Takriban askari 5,000 wa Jeshi la Kulinda Amani kutoka Uganda na Burundi wapo kwenye mji mkuu wa Somalia, Mogadishu kuilinda serikali ya mpito iliyo madarakani. Jeshi hilo limejikuta kwenye mapigano na wanamgambo wanaodhibiti eneo kubwa la Somalia ya kati na kusini.

Watu hao waliofariki walikuwa wanaangalia mechi katika eneo maarufu lijulukanalo kwa jina la Kabalagala and kwenye klabu ya rugby ijulikanyo kwa jina la  Kyadondo. “Watu 64 wamethibitishwa kufariki,“ alisema Fred Opolot, msemaji mkuu wa kutoka kitengo cha uhusiano wa umma cha serikali ya Uganda.

Pia alisema watu wengine 57 wamekimbizwa Hospitali ya Taifa ya Mulago  baada ya kupata maumivu makali, huku wengine 14 wakiwa wamepata majereha madogo madogo. Rais Yoweri Museveni  wa Uganda, ambaye alitembelea eneo la tukio, alistushwa na habari za milipuko hiyo na jana alitarajiwa kutembelea hospitalini hapo kuwaona majeruhi wa ajali hao Msemaji wa polisi Judith Nabakooba alisema uchunguzi unaonyesha unatilia shaka  kikundi cha wapiganaji wa kiislamu Al-Shabab nchini Somalia ambako Uganda imetuma majeshi yake kusaidia katika shughuli ya amani chini ya Umoja wa Afrika.

{youtube}ggTZQYrkZA4{/youtube}

Kundi hilo ambalo linatuhumiwa kuwa na uhusiano na Al Qaeda lilipongeza mashambulio hayo, lakini likakataa kujihusisha na mauaji hayo ya raia wasio na hatia.

Karibu watu 74 walikuwa wamekusanyika kuangalia mechi hiyo ya mwisho ya Kombe la Dunia na milipuko ilitokea kwa wakati mmoja katikati ya mechi hiyo iliyoisha kwa Hispania kushinda kwa bao 1-0 na kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza kwenye historia yake.

Milipuko hiyo imetokea siku mbili baada ya kamanda wa al-shabab kuagiza mashambulizi nchini Burundi na Uganda, nchi mbili ambazo zimetuma wanajeshi wake nchini Somalia kusimamia amani. Mashambulizi mawili kwa wakati mmoja ni moja ya tabia za kundi la Al Qaeda.  Hussein Issa, Nibwene Naighty na mashirika ya habari.

{youtube}DCbThJ3037Q{/youtube}

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents