Burudani

Uongozaji wa video ni cheo kidogo sana kwenye industry yangu – Nisher

Muongozaji wa video kutoka Arusha, Nisher amefunguka kwa kudai kuwa kutokana na vitu vingi ambavyo anafanya katika tasnia ya burudani, uongozaji wa video anaupa nafasi ndogo katika maisha yake.

Nisher ambaye ametoa vichupa vikali kama Xo ya Joh Makini, Bongo Hip Hop ya Fid Q nadhalika, ameimbia Lake FM kuwa kumchukulia kama director tu sio sawa.

“Kila mtu ana opinion yake kuhusu Nisher, kama umeanza kunifutilia I don’t call myself like director au Nisher is director,” amesema na kuongeza. “Director ni cheo kidogo sana kwenye industry ya nisher, mimi ni producer, director, sound engineer na recorder engineer”.

Mwezi mmoja uliopita Nisher alitoa wimbo wake uitwao Sio Mbaya, na pia ndiye aliyesimamia wimbo wa Fid Q ‘Bendera ya Chuma’ aliomshrikisha Ben Pol. Pia alishaingiza katika filamu yake fupi ‘Alex’.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents