Michezo

Uongozi wajuu wa TFF mikononi mwa TAKUKURU

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania, (Takukuru) imethibitisha kumshikilia Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi pamoja na katibu wake, Mwesigwa Celenstine kwa mahojiano ambayo hakuyaweka wazi.

Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Mussa Misalaba akizungumza na wanahabari

Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Mussa Misalaba amethibisha kuwa viongozi hao walikamatwa kwa ajili ya uchunguzi ambapo amesema kuwa Jamal Malinzi na wengine wanaendelea kuhojiwa kwa tuhuma mbalimbali.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tuhuma mbalimbali dhidi yao kuhusu matumizi mabaya ya fedha za Taasisi hiyo ya kitaifa na kusemekana Takukuru ilikuwa kwenye uchunguzi dhidi yao kwa muda sasa mpaka jana walipoamua kuwatia nguvuni.

Kuhusu ufafanuzi wa tuhuma hizo, ofisa huyo alikataa kuzitaja kwamba ni suala la kiuchunguzi.

Misalaba ameshindwa kuelezea lini viongozi hao watafikishwa mahakamani nakusema hawezi kusema kwakuwa inawezekana kama watuhumiwa hao wakitoa ushirikiano kwa Takukuru wa ushahidi wanaweza wasifikishwe mahakamani.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents