Habari

Upasuaji wa tatu wa kuwekea uume kuwahi kufanyika wafanywa kwa mzee mwenye miaka 64 Marekani

Mzee mwenye umri wa miaka 64 aliyekuwa amepoteza uume wake kutokana na saratani, anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji wa kwanza wa kumwekea uume mwingine nchini Marekani.

doctor+surgery+hospital

Upasuaji huo ulidumu kwa saa 15 mapema mwezi huu kwenye hospitali ya Massachusetts na unakuwa wa tatu wa aina hiyo duniani. Madakrari wamedai kuwa uume wa mzee huo ulioacha kufanya kazi mwaka 2012 utarejea kwenye afya yake.

Uume huo mpya ulitolewa kutoka kwa mtu aliyefariki ambaye ana aina moja ya damu na Mzee huyo aitwaye Thomas Manning. Manning, ambaye hakuwa kwenye uhusiano wakati amebainika na ugonjwa huo anasema alilazimika kukaa ili kujisaidia haja ndogo na alikuwa akiogopa kuwa na uhusiano na mwanamke.

Upasuaji wa kwanza wa aina hiyo ulifanyika China mwaka 2006 lakini uliondolewa baadaye kutokana na tatizo kubwa la kisaikolojia kwa mtu huyo pamoja na mke wake. Upasuaji uliofanikiwa zaidi ulikuwa ni wa Afrika Kusini baada ya kijana mwenye miaka 21 kuwekewa uume mwingine baada ya kuathirika na tohara mbaya.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents