Burudani

Update:Wabunge Ester Bulaya na Halima Mdee walichoongeza kusema kuhusu kuvalia Kesi ya ‘Lulu’,njuga


Baada ya wabunge, Halima Mdee wa Chadema na Ester Bulaya wa CCM kumtembelea msanii anayeshikiliwa kwa kesi ya maujai ya Kanumba, Elizabeth Micheal aka Lulu, waheshimiwa hao wamefunguka zaidi kwa nyakati tofauti uamuzi wao wa kumsaidia msanii huyo ambaye kwa sasa yuko Magereza ya Segerea.

Mh. Halima Mdee mapema wiki iliyopita, aliweka wazi dhamira yake kuhakikisha Lulu amepata mwansheria na pia kuomba Watanzania kusaidia kwa hali na mali familia ya Lulu ambayo kwa kiasi kikubwa ilikua inamtegemea yeye.

Halima Mdee, alisema,


Baada ya kupokea maswali mengi kupitia watu tofauti kutaka kujua kwanini Mbunge huyo ameamua kuvalia kesi hii ya Lulu njuga, Mdee jana aliongezea kwenye uurasa wake wa Twitter na kusema kwamba,

Mh. Ester Bulaya, akiongea na Bongo5 amesema kwamba, kesi hiyo imeamsha hisia kubwa sana kitaifa, na kwake yeye ilimgusa pia, kama Mtanzania, Kiongozi,Mbunge Kijana,mwanamke na pia mpenzi ya tasnia ya filamu Tanzania.Mh. bulaya amesisitiza kwamba angependa kuona haki inatendekea kwa Lulu, na sheria ichukue mkondo wake, ingawa hakuna anayeweza kuelewa kilichotokea usiku ule,Kanumba alivyofariki.

‘Hakuna mtu anayeweza kujua kilichotokea chumbani usiku ule na kupelekea kwa Kifo cha Kanumba. Mimi na Mh. Halima Mdee tulikwenda kumtembelea Lulu polisi, sio kwa kuchagua upande mmoja na kusherekea kifo cha Kanumba kama vile baadhi ya vyombo tofauti vilivyoandika. Tulitaka kumuona binti huyo ambaye kwanza ni bado ni mdogo kisheria na pia, kumfanyia counselling ya kisaikologia,kwani alikua analia sana na alikua ameshtuka kwa kilichotokea sana. Hali ingeweza kuwa tofauti usiku ule na Lulu tungempoteza na Kanumba angebaki pia nisingesita kutoa support kwake.’

Mh. Bulaya amesisitizai watu kutokua wepesi kumhukumu Lulu na kumuachia apate nafasi yake ya kuelezea upande wake mbele ya vyombo vya sheria.

Kesi ya Lulu, inatarajiwa kusikilizwa tena tarehe 23/04/12

mbunge kijana, mbujnge mwanamke

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents