Habari

Update: Majeruhi wa Lucky Vicent waliopelekwa Marekani kuendelea kusoma huko

Majeruhi wa ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent mkoani Arusha waliopelekwa nchi Marekani kwa ajili ya matibabu inaelezwa hali zao kuendelea kutengamaa na wiki ijayo watanza kusoma kufuatana na mtaala wa shule yao.

Wilson akionyesha tabasamu mara baada ya matibabu

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu akizungumza na Clouds Fm amesema kwa sasa anatokea bungeni na moja kwa moja anaelekea Arusha kuonana na mkuu wa mkoa huo, na baadae ataenda shule ya Lucky Vicent kuona nini cha kufanya.

“Watoto wale wengine wawili Wilson na Sadia wamekamilisha huduma za upasuaji bado wapo katika vyumba vyao katika hospitali, lakini wameshaanza mazoezi ya viungo.

“Tumejadiliana jana  na madaktari mpaka kufikia wiki ijayo itakuwa vizuri wanapofanya mazoezi watoto hawa watakuwa wanapewa muda mfupi kila siku kujifunza. Tunataka waendelee kufundishwa ile syllabus ambayo walikuwa wanatumia shuleni kwao, watapata waalimu wa kujitolea ambao watajifunza ule mtaala na waendelea kuwafundisha kidogo kidogo wakati wapo kwenye hatua za kupona kabla hawajarudi nyumbani,” amesema na kuongeza.

“Baadae nitapita kwenye hiyo shule nione mtaala wao, nionane na walimu wanaowafundisha hapa Tanzania niweze kuwaunganisha na wale wanaowafundisha kule kwenye matibabu Marekani  ili wapate huduma zote watakapo kuwa wanafika basi wataungana na wenzao shuleni all most wakiwa wapo pamoja,” amesema Nyalandu.

Ameongeza kuwa Doreen leo anaingizwa katika upasuaji mwingine, na taarifa za awali alifanyiwa upasuaji juzi kwenye nyonga na ulifanikiwa, upasuaji wa pili ulifanyika kwenye bega na kufanikiwa. Upasuaji wa tatu ulikuwa kwenye kidevu ambapo alifanyiwa na madaktari watutu kwa masaa manne akawa amechoka sana wakampa muda wa kupumzika.

“Na siku ya leo majira ya saa 10 kwa muda wa Tanzania, Doreen atafanyiwa upasuaji wa uti wa mgongo ambao wanasema unafacture lakini madaktari wamesema leo mapema asubuhi kwamba upasuaji ule utakuwa ni mgumu. Madaktari bingwa watatu watashiriki katika upasuaji huo, kwa kweli wamesema sisi kama Watanzania wote tuwaombee   wadaktari wafanikiwe,” ameeleza Nyalandu.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents