Habari

Update: Taarifa zilizotufikia kuhusu msiba wa mama yake Pink

Baada ya hapo jana jioni kutokea kifo cha mama wa rapper Pink, taarifa nyingine zimetufikia kuhusu msiba huo.

Akiongea na Bongo5 Jumapili hii, meneja wa rapper huyo, Mbezi amesema marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumanne baada ya kuwasili kwa ndugu zake kutoka maeneo mbalimbali.

“Msiba upo maeneo ya Tabata Chang’ombe nyumbani kwa babu wa marehemu. Lakini kwa sasa wanasubiriwa ndugu wa marehemu wanaotarajiwa kufika leo na kesho ambapo siku ya Jumanne ndio wanatarajia kuzika hapa hapa Dar es Salaam, nahisi itakuwa katika makaburi ya Tabata,” amesema.

Endelea kukaa karibu nasi tuendelee kukupa taarifa zaidi za msiba huo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents