Habari

Updates: Abiria wa ndege ya Kenya Airways iliyotua kwa dharula Athens, Ugiriki Jumamosi (July 6) bado wamekwama mpaka sasa

Abiria waliokuwa wakisafiri na ndege ya shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways (KQ) iliyotua kwa dharura katika uwanja wa ndege wa Athens Ugiriki Jumamosi iliyopita (July 6), wamekwama baada ya mamlaka ya anga ya Ugiriki kuizuia ndege hiyo kuondoka toka Jumamosi ilivyotua uwanjani hapo.

KQ

Katika taarifa iliyotolewa leo Jumatatu (July 8) na uongozi wa KQ na kuripotiwa na Standard Digital, ndege hiyo ilipangiwa kuondoka jana Jumapili saa 3 usiku lakini iliahirishwa tena kuondoka katika dakika za mwisho kabla ya muda huo.

“This follows the denial of clearance by the Greece Civil Aviation in spite of approval by Kenya Civil Aviation Authority and the manufacturers, Boeing, for reasons yet to be officially communicated,” alisema Chief Operating Officer wa KQ, Mbuvi Nguze.

Nguze aliendelea kusema KQ inafanya utaratibu wa kuwasafirisha abiria 301 waliokwama huko Athens kuja Nairobi kwa ndege ambayo iko tayari kutoka Nairobi, inayosubiri kuruhusiwa na mamlaka ya Anga ili kuwasafirisha abiria hao, “We have an aircraft in Nairobi ready, and crew is on hand awaiting regulatory clearance to commence the mission,” Alisema.

Pamoja na utawala wa KQ kuwahudumia abiria wote kwa kuwalipia hoteli pamoja na gharama zote huko Athens, abiria hao wemeelezea kusikitishwa kwao kupitia mitandao ya kijamii.

Ndege ya KQ 117 iliyokuwa ikitokea Amsterdam ikielekea Nairobi Jumamosi (July 6) ilitua kwa dharula mjini Athens, Ugiriki baada ya ishara ya tahadhari ya moto kutokea katika eneo la mizigo na kusababisha abiria 301 waliokuwa katika ndege hiyo kukwama.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents