Updates kifo cha Sharo Milionea: King Majuto presha yampanda, soma meseji ya Sharo iliyoashiria utabiri wa kifo chake

Leo ni siku ngumu kwa mashabiki wa msanii, muigizaji na mchekeshaji maarufu nchini, Sharo Milionea aliyefariki kwa ajali mbaya ya gari alilokuwa akiliendesha kutokea Dar es Salaam kwenda Muheza, Tanga jana majira ya saa mbili usiku.

Kifo hicho kimewastua wengi lakini zaidi ni kwa Mzee Majuto ambaye yeye na marehemu walikuwa wametengeneza ‘chemistry’ isiyo na kifani kutokana na kuigiza filamu pamoja na matangazo ya biashara kama mtu na mwanae.

Inadaiwa kuwa baada ya kupata taarifa hizo, King Majuto alipandwa na presha ambapo kwa mujibu wa EATV alikuwa na hali mbaya kutokana na mshtuko huo.

Mjomba wa marehemu Sharo Millionea, Bwana Omary Fundikira amesema marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho, Jumatano. Hii ni kutokana na msanii mwenzake John Maganga kuzikwa leo.

Katika hatua nyingine kwenye mitandao ya kijamii kumesambaa ‘screen shot’ ya meseji ya mwisho aliyokuwa akichat na rafiki yake ambayo inasomeka Sharo akisema, “Nimekurupuka tu kaka cpo poa kama nimerogwa hivi. Kuna hela nampelekea mama then narudi tufanye yetu.” Rafiki yake alimsihi aendeshe kwa umakini kwa kumwambia, “Poa kuwa makini road.”

Nao wasanii mbalimbali pamoja na watu maarufu nchini wamekuwa wakielezea kwenye mitandao ya kijamii jinsi walivyoshtushwa na kifo chake:

Adam Mchomvu

danm this jamani daah? Kama ndoto ama story ila ina baki kuwa ukweli the dude is gone, never came back (sharo milionear)… kapumzike kwa amani ma men u played ur part so much in ur life time , u made us lough, happiness, feel good when u do yo thng, amsha amsha type of music yaani daaah!

Anselm Soggy The-Entertainer

Leo nimezidi kuwa muoga…..KAMA KUNA YOYOTE NIMEWAHI KUMKWAZA NAOMBA ANISAMEHE

Fid Q

Wengi wetu leo baada ya KUAMKA kitu cha kwanza tulichofanya ni kumshukuru Mungu kwa kuiona SIKU MPYA.. *Naomba tusiusahau huu utaratibu.

AY

R.I.P Sharo Millionea,Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi,Poleni sana Familia,jamaa na marafiki

Profesa_Jay

Daaah yaani hata bado siamini, naona kama sio kweli hivi ingawa ukweli ndio huo, Mwenyezi mungu akupumzishe kwa AMANI, Gone too soon SHALO!!

Vanessa Mdee

Sharo Millionea, Rest in Eternal Peace

DJ CHOKA

Ulivyoanza game watu walikuwa kama hawakuelewi wengine kukucheka na wengine kukuita mshamba na hata tv walikuwa wanazima..sasa ndio kwanza mafanikio yalikuwa ndio yanasogea ndugu yangu lakini kazi ya mola haina makosa kichaa wangu. Nenda mwana kapumzike sasa umetuacha kila mtu atakupenda na utakuwa star upya na kunawengine watakula kwa mgongo wako ila baridaa ndio life ya kibongo. RIP

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents