Soka saa 24!

Updates: Lulu hajatoka kwa dhamana, kesi yake itahamia Mahakama Kuu

lulu  22

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwandishi wa habari wa Clouds FM, msanii wa filamu Elizabeth Michael maarufu Lulu hajatoka nje kwa dhamana bali kesi yake iliyosikilizwa leo kwenye mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam itahamishiwa kwenye mahakama kuu ya Tanzania.

Hiyo ni kutokana na mahakama ya Kisutu kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi za mauaji na hivyo jalada la kesi ya Lulu katika mahakama hiyo limefungwa rasmi leo.

Awali kulikuwa na taarifa katika mitandao mbalimbali nchini kuwa mahakama imempa dhamana muigizaji huyo anayekabiliwa na kesi ya mauaji dhidi ya Steven Kanumba.

Kutokana na maamuzi ya leo, Lulu ataendelea kubaki gerezani Segerea mpaka pale mahakama kuu itakapopanga tarehe ya kuanza kusikilizwa kesi yake katika mahakama hiyo.

Leo mashahidi zaidi ya sita wametoa ushahidi wao mahakamani hapo akiwemo yeye mwenye Lulu aliyesimulia jinsi tukio hilo lilivyokuwa.

Related Articles

Back to top button
Bongo5

FREE
VIEW