Habari

Updates: Majeruhi wa Lucky Vicent wako tayari kurejea nyumbani

Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amesema kuwa majeruhi wa shule ya Lucky Vicent ya jijini Arusha ambao walikuwa nchini Marekani kimatibabu kufuatia ajali iliyotokea jijini Arusha wako tayari kurejea nyumbani nchini Tanzania.

Hayo yamebainishwa leo na mbunge Nyalandu kupitia mtandao wake instagram ambapo amekuwa akitoa huku akiwashukuru Watanzania wote kwa sala na dua.

Ready To come home! Watoto wetu Doreen, Sadia na Wilson sasa wako tayari kurejea nyumbani. Mungu awabariki wote kwa Sala na Dua zenu. Hakika Mungu akitaka kukubariki, hakuna awezaye kuzuia! Amani iwe nao! Sote tujimuike kuwapokea KIA asubuhi saa 3.00 Ijumaa ya wiki hii. Ndege aina ya DC-8 itawarejesha nchini, na watu wote wanatarajiwa Kufika airport saa 7 asubuhi. Mgeni Rasmi atafika saa 2 asubuhi, na watoto watatua saa 3 asubuhi. Leo ntatoa RATIBA nzima ya HAFLA ya airport KIA.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents