Upigwaji marufuku wa vipanya

VipanyaNapenda kuchukua nafasi hii kushukuru website yenu kwa kutupa sisi
wananchi nafasi ya kutoa maoni yetu kutokana na mambo yanayotokea
katika jamii yetu ya watanzani na nchi yetu kwa ujumla

Napenda kuchukua nafasi hii kushukuru website yenu kwa kutupa sisi wananchi nafasi ya kutoa maoni yetu kutokana na mambo yanayotokea katika jamii yetu ya watanzani na nchi yetu kwa ujumla.

 

Kwanza napenda kukufahamisheni kwamba mimi si mwandishi wa habari ila huwa naguswa sana na mambo mbali mbali yanayotokea katika nchi yetu kutamani kutoa maoni yangu juu ya mambo hayo.

 

Kikubwa ambacho napenda kukizungumzia katika habari yangu hii ni kuhusu Kupigwa marufuku kwa mabasi madogo madogo ya abiria maarufu kwa jina la vipanya.

 

Labda kwa vile mi si mdau hau sina uelewa wa kutosha ni kwa vipi hii mamlaka ya kudhibiti usafiri wa nchi kavu na majini-SUMATRA wameamua kupigwa marufuku mabasi hayo.

 

Tukiangalia kwa upande wa usafiri kwa jiji la Dar es Salaam nadhani akuna asiyejua kama ni wa tabu kupita maelezo ingawa hivyo vipanya vipo vikisaidia kwa kiasi kikubwa katika swala zima la usafirishaji wa abiria. Sasa iwapo hawa SUMATRA watapiga marufuku vipanya ambavyo ukiangalia utaona ni vingi kuliko hayo mabadi makubwa wanatarajia sisi wananchi tunaotegemea usafiri wa dala dala tutafanya nini.

 

Kwa kiasi kikubwa vipanya vinasaidia sana katika usafirishaji wa abiria sehemu mabali mbali za miji katika nchi yetu.
Hivyo tunaomba Sumatra ifikirie swala hili kwa urefu isiwe kwa vile wao wana usafiri wao binafsi wa kuwatoa majumbani mwao na kuwapeleka sehemu mbali mbali za shughuli zao wakurupuke tu katika suala hili.

 

Pia tungependa kama inawezekana wakaandaa kipindi iwe redioni ama kwenye television ili wananchi waweze kutoa maoni yao juu ya suala hili, na sio kuwalazimisha wananchi wakubaliane na uwamuzi wao kwa kutoa matangazo yao kwenye redio yenye lengo la kuwashawishi wananchi wakubaliane na mpango wao.

 

Kutoka kwa Mdau Stella 

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents