Habari

Upimaji VVU bado hauridhishi Zanzibar – SMZ

Wizara ya Afya Zanzibar imesema ushiriki wa jamii katika upimaji wa Virusi vinavyosababisha Ukimwi bado ni mdogo ikilinganishwa na mataifa mengine duniani.

Akizungumza mjini Unguja katika mkutano wa wadau wanaopambana na VVU, Waziri Afya Zanzibar, Mahmuod Thabit Kombo, amesema miongoni mwa sababu zinazopeleka ushiriki huo mdogo ni wanaume kutojitokeza kupima afya zao pamoja na wenzi wao.

“Shirika la afya Duniani limesema, kila mwanaume akitoa ushirikiano kwa mkewe tutaweza kupunguza maradhi takribani yote duniani kwa asilimia 50,” alisema Kombo.

“Wenzetu Bara wametushinda sana, wanaume wa bara wametushinda wanaume wa Zanzibar, kwani wao wanaojitokeza ni asilimia kubwa zaidi kufikia asilimia 80 na malengo yao watayafikia hivi karibuni wakati sie bado tuko nyuma kwa asilimia 5 , katika upimaji wa VVU bado hauridhishi vizuri.”

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents