Habari

Upinzani waahirisha sherehe za kumuapisha Raila Odinga kama Rais wa Kenya

Umoja wa Muungano wa vyama vya upinzani nchini Kenya (NASA), umetangaza kuahirishwa kwa sherehe za kumuapisha kiongozi mkuu wa umoja huo, Raila Odinga na Stephen Kalonzo Musyoka, kama Rais na Makamu wake wa Jamhuri ya Kenya.

Katika taarifa iliyotolewa jana na Muungano huo siku ya jana imeeleza kuwa imeahirisha sherehe hizo hadi itakapotangazwa tarehe hapo baadae.

Shughuli hiyo ilipangwa kufanyika Jumanne hii ya tarehe 12 Desemba 2017, ambapo NASA walisema kuwa Odinga ataapishwa kama Rais wa watu wengi.

Raila Odinga alijiondoa kwenye kinyang’anyiro cha marudio ya uchaguzi mkuu ambayo yalifanyika tarehe 26 mwezi Oktoba mwaka huu ambapo Uhuru Kenyatta aliibuka mshindi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents