Michezo

URA ya Uganda yachukua ubingwa wa Mapinduzi Cup

Timu ya URA ya Uganda imetwaa ubingwa wa michuano ya Mapinduzi Cup kwa msimu wa 2016 kwa kuifunga timu ya Mtibwa Sugar, mabao 3-1.

????????????????????????????????????

URA walianza kupata goli lao la kwanza kupitia Julius Ntambi aliyeunganisha mpira wa krosi na goli hilo kudumu mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika.

????????????????????????????????????

Katika kipindi cha pili timu hiyo ikaongeza mabao mengine mawili kupitia kwa Peter Lwasa katika dakika ya 85 jingine dakika ya 88 akimalizia pasi ya Julius Ntambi na kuwahakishia ubingwa.

Jaffar Salum aliifungia timu yake ya Mtibwa bao pekee la kufutia machozi. Hivyo kuifanya URA kuondoka na kitita cha shilingi milioni 10, na kuwa timu ya pili ya Uganda kutwaa taji hilo, baada ya KCCA mwaka 2014.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents