Michezo

Uruguay vs Ureno ni vita ya Ronaldo dhidi ya Luis Suarez

Hatua ya makundi ya michuano ya kombe la dunia imemalizika hapo jana siku ya Jumatano na timu kadhaa zikipata nafasi ya kutinga hatua ya 16 bora huku tukishuhidia bingwa mtetezi Ujerumani akiungana na vikosi vya Afrika kuyaaga mashindano hayo yanayoendelea kutimua vumbi huko nchini Urusi.

Ureno inayoongozwa na mchezaji bora duniani, Cristiano Ronaldo imetinga hatua hiyo baada ya kutoka sare ya bao 1 – 1 dhidi ya Iran kwenye mchezo wake wa mwisho na hivyo kukutana na Uruguay ya nyota wa Barcelona, Luis Suarez hapo kesho siku ya Jumamosi ya Juni 30 ambayo haijaruhusu goli hata moja langoni kwake katika kundi A.

Mchezo wa huu wa Uguay dhidi ya Ureno unatarajiwa kuvuta hisia za waliyowengi hasa wapenzi wa soka kwa namna utakavyo kuwa na mvuto wa wachezaji waliyopo kwenye kila timu huku wengi wakitarajia kushuhudia mechi yenye kushambuliana kutokana na nyota zake kuwa wenye vipaji.

Uruguay ikiwa chini ya nyota wake Luis Suarez na Edinson Cavani imeweza kuibuka na pointi tisa kwenye michezo ya kundi A, baada ya kuifunga Misri goli 1 – 0, Saudi Arabia 1 – 0 na kisha kuibuka na ushindi mnono dhidi ya wenyeji Urusi kwa jumla ya mabao 3 – 0.

Kwa upande wa Ureno, Ronaldo aliiyongoza kuibuka sare ya mabao 3 – 3 dhidi ya Hispania, ushindi wa goli 1 – 0 na Morocco kisha sare ya 1 – 1 na Irani.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents