Habari

URUSI: Ndege yatua kwenye shamba la mahindi baada ya kuvamiwa na kundi la ndege

Ndege ya abiria ya Urusi imelazimika kutua kwa dharura kwneye shamba la mahindi karibu na jiji la Moscow baada ya kugonga kundi la ndege.

Watu ishirikini na watatu wamejeruhiwa katika tukio hilo, ambalo limesababisha ndege kutua huku injini yake ikiwa imezima na gia yake kutua ikirudi nyuma, wamesema maafisa wa afya.

Ndege hiyo Ural Airlines Airbus 321 ilikuwa ikisafiri kuelekea katika eneo la Simferopol Crimea ilipogonga kundi la ndege muda mfupi baada ya kuondoka uwanjani , hali iliyovuruga utendaji wa injini yake.

Ndege ilikuwa na abiria 233 p na wahudumu ndani yake ilipolazimika kutua kwa dharura

Vyombo vya habari vya taifa la Urusi vimetaja kutua kwa ndege hiyo kama “muujiza wa eneo la Ramensk”.

Maafisa wa ndege hiyo wamesema ndege imeharibika sana na haiwezi kupaa tena. Uchunguzi rasmi juu ya ajali hiyo unaendelea.

Kwa mujibu wa mashirika ya habari ya  The Mosco TimesReuters na BBC, Ndege hiyo ilikwa na abiria 233 na wahudumu ndani yake wakati ndege waliporipotiwa kuingia ndani ya injini na rubani wake akaamua kutua mara moja.

Abiria mmoja ambaye hakutajwa jina lake ameiambia televisheni ya taifa kuwa ndege ilianza kuyumba kwa hali ilisiyo ya kawaidabaada ya kuondoka uwanjani.

“Sekunde tano baadae, taa za upande wa kulia za ndege zikaanza kuwaka na kuzima na kulikuwa na harufu ya kuungua . halafu tukatua na kila mtu akatimu mbio kwenda mbali ,” alisema.Wasafiri na wahudumu wa ndege waliondoshwa haraka kutoka eneo la tukio baada ya ndege kutua kwa dharura

Wasafiri na wahudumu wa ndege waliondoshwa haraka kutoka eneo la tukio baada ya ndege kutua kwa dharura

Shirika la usafiri wa ndege la Rosaviatsia limesema kuwa ndege hiyo ilitua katika sahamba la mahindi yapata kilomita moja (maili 0.62 ) kutoka kwenye njia yake kwenye uwanja wa kimataifa Zhukovsky , huku injini yake ikiwa imezima na breki zake za kutua zikiwa zimerudi nyuma .

Wasafiri waliondoshwa kutoka kwenye ndege , huku baadhi wakipelekwa hospitalini kwa matibabu na wengine wakiongozwa kuelekea kwenye uwanja wa ndege.

Wizara ya afya imesema kuwa watoto watano walikuwa miongoni mwa wasafiri waliolazwa tkufuatia ajali hiyo.. Wale waliojeruhiwa katika mkasa huo walichukuliwa kama watu wenye “hali mbaya na hali ya kawaida “,imesema.

Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya ndege ya Ural Airlines Kirill Skuratov amewaambia waandishi wa habari kuwa wasafiri waliotaka kuendelea na safari yao watawekwa kwenye ndege mbadala baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu.

Vyombo vya habari vya Urusi vimelinganisha tukio hilo na tukio la safari ya ndege ya Marekani-US Airways iliyolazimika kutua kwa dharura katika mto Hudson muda mfupi baada ya kupaa mnamo mwaka 2009.

Migongano baina ya ndege na ndege ni jambo la kawaida katika safari za anga , huku maelfu ya ajali hizo zikitokea nchini Marekani pekee. Hata hivyo, ni nadra kusababisha ajali au kusababisha uharibifu kwenye ndege.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents