Habari

URUSI: Utafutwaji wa Tanzania mtandaoni waongezeka mara 65 kisa Utalii, Waziri Kigwangalla atia neno

Uperuzi wa Taifa la Tanzania mtandaoni umeongezeka mara 65 nchini Urusi baada ya Naibu Waziri Mkuu, Tatyana Golikova kutangaza kuwa nchi hiyo itarejesha safari za ndege za Tanzania kuanzia Agosti 1, 2020.


Kwa mujibu wa Yandex, Ijumaa ya Julai 24, maombi ya kulitafuta Taifa la Tanzania mtandaoni yaliongezeka mara 65 ikilinganishwa na siku ya nyuma yake, Alhamisi Julai 23.

Inaelezwa kuwa Watumiaji wa Yandex waliperuzi zaidi kuhusu eneo la Kijiografia la Tanzania, jinsi nchi inavyoonekana, safari za ndege, maoni mbalimbali kutoka kwa watalii pamoja na hali ya hewa.


Siku ya Ijumaa, Serikali ya Urusi ilitangaza kuanza tena kwa safari za ndege na Uturuki, Uingereza na Tanzania kuanzia Agosti 1 ambapo kuingizwa kwa Tanzania ni kwa sababu ya umaarufu wa nchi hiyo kwa Watalii.

https://www.instagram.com/p/CDRBj5iJ0IH/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents