Michezo

Urusi vs New Zealand kombe la Mabara kuanza leo

Mashindano makubwa ya Mabara yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi hii leo Urusi ikiwa ni kabla ya mwaka mmoja kufanyika kwa fainali za kombe la dunia nchini humo.

Kuelekea Michuano hiyo Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulimwenguni (FIFA) limewataka waamuzi wote watakaochezesha  kusimamisha mchezo endapo Mashabiki watatoa Lugha za kibaguzi wakati wa Mechi.

Wenyeji hawa wa michuano ya Mabara pamoja na Kombe la Dunia mwaka 2018  hawana sifa nzuri juu ya matendo ya kibaguzi uwanjani na mara nyingi kumekuwa pakizuka vurugu za mara kwa mara kitendo kinacho sababisha FIFA kuweka waangalizi wake wa masuala ya kibaguzi viwanjani.

Urusi iliyo katika kundi A, leo itajitupa uwanjani katika mchezo wa ufunguzi kwa kuwakabili New Zealand wakati timu ya taifa ya Ureno ikiwakabili Mexico siku ya Jumapili.

BY HAMZA FUMO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents