Habari

Urusi yatetea haki ya Iran, yawasilisha barua nzito kwa Katibu Mkuu Umoja wa Mataifa

Urusi inatetea haki ya Iran ya kurusha setilaiti na kupuuza madai ya Marekani kwamba Iran inakiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa kuhusu makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015 kati ya Iran na mataifa sita yenye ushawishi mkubwa kwa kurusha setilaiti hiyo angani.

Katika barua iliyowasilishwa jana kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Gutteres na baraza la usalama la Umoja huo, mjumbe wa Urusi katika Umoja huo Vassily Nebenzia, amesema kuwa juhudi zinazoendelea za Marekani kuinyima Iran haki ya kufurahia manufaa ya teknolojia ya amani ya angani chini ya kisingizio cha uongo ni hatua zinazoibua wasiwasi na kusikitisha.

Nebenzia ameongeza kuwa Iran haijawahi kumiliki silaha za nyuklia, wala haimiliki silaha hizo kwa sasa ama kutarajiwa kuzimiliki katika siku za usoni.

Russia defends Iran satellite launch against US opposition | The ...

Vikwazo vya silaha vya Umoja wa Mataifa dhidi ya Iran vinatarajiwa kumalizika mwezi Oktoba na Marekani imesambaza rasimu ya maamzimio ya Umoja wa Mataifa ambayo itaongeza kwa muda usiojulikana vikwazo hivyo kwa idadi ndogo ya wanachama wa baraza hilo mwishoni mwa mwezi Aprili.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents