Siasa

US Election: Obama atoa hotuba nzito baada ya ushindi

http://www.youtube.com/watch?v=nv9NwKAjmt0

Ni kawaida kwa uchaguzi wa Marekani kugusa hisia za si wamarekani tu bali hata nchi zingine duniani. Watanzania wengi hawakuwa nyuma pia, na tangu kutangazwa kuwa rais Barack Obama anarejea kwa awamu ya pili katika ikulu ya whitehouse, wengi wamefurahia kana kwamba Obama ni rais wa dunia.Imemchukua muda kidogo mpinzani wake wa chama cha Republican, Mitt Romney kushika simu na kumpigia Obama kumpongeza kwa ushindi wake, lakini hatimaye amefanya hivyo.

Akiwa ameongozana na mke wake Michelle pamoja na watoto wao wawili Sasha na Maria na kuwasili kwaajili ya kutoa hotuba yake, umati mkubwa wa wafuasi wake waliokuwa wamekusanyika jijini Chicago, Illinois ulilipuka kwa shangwe na vigelegele huku bendera za Marekani (na sio za chama chake) zikipeperushwa kuashiria umoja na mshikamano mkubwa wa nchi hiyo kubwa duniani.

“I want to thank every American who participated … whether you voted for the very first time or waited in line for a very long time, “ alisema.

Hakusita kuishukuru timu yake ya kampeni kwa kuiita, “best campaign team and volunteers in the history of politics”.

Lakini pia alimshukuru mpinzani wake kwa kusema, “Honor and applaud” the legacy of public service of the Romney family.”

“Tonight, you voted for action, not politics as usual. You elected us to focus on your jobs, not ours.”

Alisikika pia akisema anaingia ikulu akiwa na nguvu mpya zaidi ili kuhakikisha kuwa Marekani inaendelea kuwa taifa kubwa zaidi duniani.

Mara kwa mara wakati wa hotuba yake hiyo wafuasi wake walikuwa wakitoa shangwe kubwa kutokana na kuguswa na maneno yake hali inayomfanya bado aonekane kuwa miongoni mwa marais wachache wenye hotuba zenye mvuto zaidi duniani.

Unadhani Tanzania tujifunze nini kutoka kwenye uchaguzi wa Marekani?

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents