Habari

Usafiri wa InDriver kuwapa nafasi wateja wao wa Arusha kuamua bei za safari zao

Arusha, Novemba 14, inDriver, kampuni ya kimataifa ya usafiri wa njia ya mtandao wa simu yenye makazi yake jiini New York, sasa unapatikana Kwa wakazi wa Arusha.

Watumiaji wa inDriver watakuwa na uhuru wa kuchagua na kupanga bei za safari zao, huku maderevea wakichagua bei waionayo kwa umbali wa safari waionayo inafaa kwao.

Njia pekee ya kutumia usafiri wa taxi jijini Arusha, ni kujadiliana bei ya safari kati ya abiria na dereva kabla ya safari. Mteja hawezi kujua kama kuna madereva wa kutosha katika sehemu unayotoka vilevile dereva huwezi kuwa na uhakika kama kutakuwa na wateja wengi kwa siku hiyo, hivyo inDriver ni app rahisi kutumia ambapo inampa abiria uwezo wakupanga safari aitakayo. Kwa madereva, inDrive ni njia rahisi yakupata wateja wengi kwa kutumia simu janja (smartphone) zao; Na kwa abiria, kuweza kuchagua na kupanga bei za safari zao.

Arusha ni mji wa kwanza Tanzania na barani Afrika ambapo app ya inDriver ilizinduliwa. Huduma hii imeunganisha zaidi ya madereva 300 jijini Arusha na wengine wakizidi kusajiliwa kila siku. Katika hatua za mwanzo za huduma hii, inDriver haitowatoza kamisheni yoyoye madereva wake.

InDriver yampa mtumiaji uwezo wakujilinda na kuwa salama. Mtumiaji anaweza kushare na kuwaatarifu ndugu, marafiki na hata katika mitandao ya kijamii juu ya safari yake. Hii nikuwawezesha walio karibu nawe pamoja na wapendwa wako kutokuwa nawasiwasi pindi
anaposafiri. Watumiaji wanaweza kubofya “share” muda wowote katika safari zao.

Ukitumia app yetu ya inDriver, waweza safiri sehemu zozote ndani ya mkoa wa Arusha. Kwa sasa, watumiaji wataweza lipia safari zao kwa “cash” peke yake ambapo yaweza punguza gharama ikilinganishwa nakulipia kwa mtandao ambapo kuna makato ya ziada.

Wiki iliyopita, inDriver imekuwa katika majaribio mkoani Arusha ili kukusanya maoni toka kwa watu. Ilionyesha kuwa bei za safari ni bora sana kwa wasafiri. Kwa mfano, kusafiri kutoka Clock tower hadi Philips mteja alilipa shilingi elfu 3,000 tu, kutoka Mianzini kwenda
hospitali ya Mount Meru ni shillingi elfu sita 6,000 tu.

“Arusha ni kati ya miji yenye uchangamfu na ukubwa ikiwa na wakazi wenye uhitaji wa huduma ya usafiri wa haraka na uhakika. Hadi sasa, wakazi wa Arusha wamekuwa wakishindwa kupata huduma ya usafiri wa uhakika na hivyo kusumbuka kutafuta taxi katika vituo hata iwe ni msimu wa mvua.

Pia wadereva walikuwa wakishinda kukaa katika vituo vya taxi kwa masaa mengi bila kupata wateja. inDriver imekuja kubadilisha hili na kuwa suluhisho kwa tatizo la usafiri. Tunaitaji wateja na madereva kuwa na program tumishi (App) bora ya usafiri katika safari zao. Hivi sasa, watumiaji wa inDriver wataweza kuchagua safari wazatakazo kwa muda na sehemu wazitakazo.

Na siku za usoni, mikoa mikubwa mingine nchini Tanzania, wataweza kutumia progaramu tumishi hii vizuri pia.”Ygor Fedorov, Mkurugenzi kitengo cha Biashara, inDriver.

Kwa sasa, waweza pakua programu tumishi ya simu (App) ya inDriver katika Google Play Store na Appstore.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents